Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp ametania kuwa hutoonyesha ukali kwa mwamuzi wa kike Stephanie Frappart atakayechesha mechi ya leo UEFA Super Cup kati ya Liverpool na Chelsea.
Mwanamama Stephanie raia wa Ufaransa, ataweka rekodi kwa kuwa mwamuzi wa kwanza wa mwanamke kucheza mchezo huo mkubwa wa UEFA huku akisaidiwa na wanawake wenzake Manuela Nicolosi na Michelle O'Neill.
Nitajaribu kutokuwa mkali ili nisiufanye mchezo kuwa mgumu kwao. Nitaonyesha sura ya upole na upendo vinginevyo mama atachukizwa nami nyumbani," anatania jamani.
Klopp ambaye aliipa Liverpool taji la sita la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alisema anajisikia kuwa mwenye furaha kuwa sehemu ya tukio la Kihistoria ambalo litafanyika leo, Uturuki.
Alisema hatimaye muda umefika wa historia kuweka, itakuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kuchezesha mchezo mkubwa kama huo, lakini akadai haitakuwa mwisho kwa waamuzi wa kike kuaminiwa.
Frappart ambaye Aprili alikuwa mwamuzi pekee kuchezesha Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’ alisema kuna ugumu kucheza mechi ya wanaume huchangiwa na ushindani uliopo baina yao.
Najua duniani kote wanawake watafuatilia wapenda michezo kuona vile ambavyo wenzao wanaenda kuweka histotia," alisema kocha huyo ambaye timu yake ilianza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu England.
“Kante alipata maumivu kidogo katika mechi na United, ni hatari kama utaendelea kuwatumia wachezaji wa aina hii, tunahitaji kufanya uamuzi sahihi,”alisema Lampard.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.