Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

20190822_122328.jpeg
 
*PHILIPE COUTINHO NA KISA CHA MAMBA BWAWANI*

Ile Hadithi Tamu ya Phelipe Coutinho Correi Almaarufu Kama Coutinho sasa Imehamia Kule Ujerumani Kunako katk Viunga Vya Allianz Arena Ndani ya Jiji la Munich

Hadithi hii iliyopambwa na Visa Vitamu Vinavyotukumbusha ile hadith tamu ya Mamba Katka Bwawa aliyejiona Mkubwa kushinda Bwawa na Viumbe Vyote ndani yake Na kutaka Ufalme Asiostahili akisahau Kama kuna wakubwa zaid kama Kiboko basi inalandana na Hadith hii ya Phelipe Coutinho Kijan Mweny Kipaji Cha Ajabu na cha Kipekee Licha ya Umbo dogo kama Alilowahi Kuwa nalo Baba yake ambaye alikuw ni Mchorji Mbobezi wa Ramani Za Majengo kule Rio de Janeiro Kipind hicho Coutinho akiwa anahangaika Kuonyesha nini Anacho mguuni katika klabu ya Vasco da Gama hiyo ilikuwa ni Mwaka 1999 mpka mwaka 2008

Babayake Ni Fundi wa Kuchora Ramani za Majengo ambay yanalipamba jiji la Rio de Janeiro Mtoto Amabaye ni Phelipe yeye ni fundi wa kuchora ramani Wapi Mpira upite na kwa wakat gani huyo ndiye Phelipe Coutinho Correia

Hadithi ya Coutinho ilizidi Utamu baada ya Kuhamia Ulaya ambapo ni ndoto ya kila Mwanasoka anatamani kufika na kuionyesha dunia nini anacho Sasa baada ya Coutinho kufika Ulaya Internationale de Milano (Inter Milan) wakavutiwa na Kipaji chake na Na kumsajili na Coutinho Akapata nafasi ya kuionyesha dunia nn anacho Na hatimaye "The Kops"
Liverpool wakamnasa Na kijana akatua An field na hapo hiyo ilikuwa ni Mwaka 2013 hadith ya Mamba na Bwawa ikaawa hadithi ya Coutinho naLiver pool

Ubora wa Kipaji chake kamwe haujawah kujificha Philipe ni Mchezaji wa kiwango cha dunia Ama wazungu wanaita "World Class Players" Ndani ya Miaka mitano na magoli 41 katika mechi 152 zilimtosha Phelipe Coutinho aamini Sasa ni Mchezaji mkubwa Zaidi ya Klabu na ulikuwa ni muda wake sahihi wa yeye kuanza kuingia kwenye Ballon d'or na Kupambana na Messi na Ronaldo na yotehaya yasinge timia bila kuwa na Ubingwa wa Uefa na akaona Liverpool sio sehemu sahihi kwake Kiburi ,Kuamini kipaji Chake mwisho kufosi uhamisho Wake kuelekea Camp Nou Nyuma Akisahau kilichowahi Kumkuta Fernando Torres "El Nino" Alipo fosi uhamisho wake kuelekea Chelsea

Sasa yup Bayern Munchen kwa Mkopo huku Nyuma akiwa kaacha record ya Kucheza michezo 52 na Magoli 13 licha ya kucheza timu moja na Lionel Messi ,Suarez,Ivan Rakitic na Mafundi kibao kama Arthur Mello .. Sijui bado kama anandoto tena za Balon d'or au Uefa na je atawapa Bayern Muchen kile walichokipata chini ya Arjen Robben na Frank Ribbery ?? Yetu Macho Karl Heinz Ruminnege Anajua kwa nini Coutinho yupo Pale .. Coutinho Samaki Mkubwa Ndani ya Bwawa dogo... Wazungu wanakuga kwa "Good Luck Phelipe"
 
Back
Top Bottom