Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.

jamii mbovu yenye watu wasiona staha wala haya imejengwa katika misingi maadili mabovu waliyopewa watoto toka wakiwa wadogo chambilecho samaki mkunje angali yu mbichi......
 
Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.

kumsaidia mtu asiyejisaidia wala kuupa thamani msaada wako ni sawa na 'KUJILA'
 
Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.

Naam wengi hujigamba na kujitapa sana kwamba akili zao,pesa zao,muonekano wao,kazi zao na vyeo vyao vimewawezesha kupata au kufikia mafanikio fulani katika maisha wanasahau ya kwamba yote hayo ni MAKADIRIO,REHMA na HURUMA tu ya Mwenyezimungu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…