Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kumbuka kwamba unaweza kupata kitu chochote kile unachokitaka maishani, lakini huwezi ukapata kila kitu unachohitaji kwa wakati mmoja. Rasilimali, muda na fedha mara zote ni kidogo haziwezi kukuruhusu kufanya hivyo, kwa hiyo njia pekee iliyopo ni kuchagua lengo moja kubwa na lililokuwa muhimu kuliko mengine yote, ukaelekezea rasilimali na nguvu zako zote kwalo na matokeo yake ni lazima tu yatakuwa mazuri.
 
Wana elimu ya mafanikio wengine hatua hii ya kuweka mipango katika kufanikisha malengo hutofautiana kidogo ijapokuwa wote kwa ujumla wanakubaliana katika ndoto, malengo na utekelezaji. Kuna wanaoponda suala la kuweka mipango(Plans), kwamba mtu anaweza tu kufikia mafanikio yeyote yale ilimradi tu awe na ndoto kichwani, kisha aamini kwamba ataweza kutekeleza ndoto hiyo. Swala la utekelezaji wanaamini litakuja tu lenyewe kupitia mawazo ya ndani na nguvu kuu ya asili(Mungu)
 
Wanasema kuweka mipango au malengo maana yake, tayari ni mambo unayoamini unayaweza, hivyo siyo lengo lenye changamoto tena. Kwa upande mwingine, wengine wanaamini huwezi ukafikia mafanikio pasipo kwanza kuwa na mipango madhubuti. Kwa mfano huwezi ukazingatia jinsi ya kupanga bajeti au kubana matumizi wakati unapotaka kutimiza mipango ya maisha au malengo ya biashara kama huelewi namna bora ya kufikia malengo hayo.
 
Mbinu za biashara mbalimbali ni lazima zihusiane na malengo na mipango hata ikiwa mtu hataki kukubaliana na ukweli huo. Kabla ya kutekeleza jambo lolote lile, kinachotangulia kwanza akilini ni malengo, kile mtu anachotaka kukifikia baada ya kutekeleza mpango huo anaoufikiria.
 
Malengo mazuri ni lazima yawe na sifa zifuatazo:-
· Yawe yanaeleweka.
· Yawe yanapimika.
· Yanatekelezeka.
· Ni ya uhakika.
· Yana muda maalumu wa kuyatekeleza.

Kwa mfano badala ya kusema, “Nataka kuwa na fedha nyingi”, sema “nataka kuwa na shilingi milioni 100 mwaka 2018”. Bila shaka lengo kama hili linaweza likatimizwa kama matayarisho ya kutosha yatafanyika.
 
Vipengele vingine muhimu mtu anavyopaswa kufuata ili kuweza kuweka malengo yanayotekelezeka ni kama ifuatavyo:-

· Andika malengo yako kwenye karatasi, kwa kufanya hivyo itakusaidia uweze kuyasoma mara kwa mara na hivyo kukaa akilini.
· Andika kila lengo kwa lugha chanya, mathalani badala ya kusema, “tutapunguza ajali”, sema, “tutazidisha hali ya usalama”
 
Eleza kwa wakati uliopo sasa, mfano usiseme, “Nitaacha kuvuta sigara” sema, “Sasa hivi naacha kuvuta sigara”


· Weka vipaumbele, ikiwa una malengo mengi, yapange kufuatana na umuhimu ukianza na yale muhimu zaidi, hii itakusaidia kuelekeza nguvu zako nyingi kwa yale malengo yaliyokuwa na umuhimu zaidi.


· Weka malengo makubwa, malengo madogo kila mtu anayaweza hivyo hayatakusisimua kuyakamilisha.(Think Big)
 
Lengo kubwa livunje-vunje katika malengo madogomadogo kusudi iwe rahisi kutekeleza.


· Usiweke malengo yasiyotekelezeka, kwa mfano, mtu binafsi kuruka kwenda sayari nyingine, kuota mabawa kama ndege, kuzunguka dunia nzima ukitembea kwa miguu nk.


· Hakikisha unadumu na malengo uliyojiwekea bila ya kukata tamaa kabisa mpaka pale utakapohakikisha umeyatimiza (Dont Give Up)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…