Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
FB_IMG_1566981347452.jpeg
 
Ian Wright

STAA wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England akiwa na umri wa miaka 19 aliwahi kufungwa jela kwa kosa la kutolipa faini kufuatia uendeshaji wa hatari wa gari. Hilo lilisababisha afungwe kwa wiki mbili katika gereza la Chelmsford mwaka 1982. Wright amewahi kuzungumzia jinsi ambavyo maisha ya gerezani yalivyombadili. “Niliwahi kusema sitarudi sehemu kama hii tena. Nilijua kwamba nilipaswa kuanza kufanya mambo yanayoeleweka bila ya kupindapinda,” alisema Wright mwaka 2016 alipokuwa anahojiwa kuhusu maisha yake ya gerezani.
 
Joey Barton

Staa huyu wa zamani wa Newcastle United aliwahi kutumikia kifungo cha siku 74 gerezani katika hukumu yake ya miezi sita jela aliyopewa Mei 2008. Barton alipatikana na hatia ya kufanya vurugu katikati ya jiji la Liverpool na akatwishwa shitaka la ‘vurugu na uhuni’ na jaji wa kesi yake. Wiki sita baadaye alipewa ongezeko la miezi minne katika hukumu yake baada ya kukiri kupigana na staa mwenzake wa zamani wa Manchester City, Ousmane Dabo.
 
adam johnson

Staa wa zamani wa Sunderland na timu ya taifa ya England, Adam Johnson, pengine ndiye mchezaji mwenye jina kubwa zaidi wa kizazi cha karibuni ambaye kesi yake ilikuwa maarufu na alifungwa miaka mitatu. Johnson alifungwa jela kwa kosa la kufanya ngono na msichana aliyekuwa na umri wa miaka 15 mwaka 2016. Msichana huyo alikuwa shabiki wake uwanjani. Kufuatia tukio hilo, Johnson ambaye ameachiwa gerezani miezi michache iliyopita alifukuzwa na klabu yake ya Sunderland ingawa amesamehewa na mkewe.
 
Duncan Ferguson

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Everton na timu ya taifa ya Scotland, Duncan Ferguson ‘Big Dun’ amewahi kukiri kwamba kitendo chake cha kukaa jela kiliharibu kabisa maisha yake ya soka. Ferguson alikaa jela kwa siku 44 kati ya miezi mitatu aliyohukumiwa kwenda jela katika gereza la Barlinnie jijini Glasgow mwaka 1995 baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga kichwa mlinzi wa klabu ya Raith Rovers, Jock McStay. Akiwa anacheza katika klabu ya Rangers wakati huo, tukio hilo lilitokea ndani ya uwanja na Ferguson alikuwa mchezaji wa kwanza wa Kiingereza kufungwa jela kwa tukio la ndani ya uwanja.
 
Tony Adams

Mlinzi huyu mahiri wa zamani wa Arsenal na nahodha aliyejipatia umaarufu mkubwa klabuni hapo baada ya kuichezea klabu hiyo kwa muda mrefu, alifungwa jela mwaka 1990 na kutumia siku 57 gerezani. Alikutwa amekunywa pombe mara 27 ya kipimo kilichotakiwa huku akiwa amepata ajali. Hata hivyo, staa huyo anakiri kwamba kukaa kwake gerezani hakukumfundisha kitu chochote. “Gereza halikunifundisha kitu chochote. Hakukuwa na elimu yoyote ya kwanini niko pale au kuhusu ugonjwa wangu. Nilijiona nipo salama na huru, kitu ambacho kilinitisha. Wakati huo sikujali chochote, lakini ilikuwa kama vile nipo hotelini,” alisema Adams.
 
Eric Cantona

Mkongwe huyu wa Manchester United alifungwa jela kwa wiki mbili katika tukio alilofanya ambalo lilishtua ulimwengu wa mashabiki wa soka. Baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika pambano la Ligi kuu ya Egland dhidi ya Crystal Palace, Cantona alimpiga teka la kung-fu shabiki mmoja wa Palace. Hata hivyo Cantona alikaa ndani kwa saa tatu tu baada ya kuwekewa dhamana.
 
Jermaine Pennant

Staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England aliyewahi kukumbana na kuta za gereza baada ya kulewa chakari mwaka 2005 na kuendesha gari lake aina ya Mercedes Benz ovyo kiasi cha kupata ajali. Alifungwa gerezani kwa miezi mitatu na ingawa alitumikia robo tu ya kifungo hicho anadai kwamba kilibadili sana maisha yake.

“Nadhani kila mtu ambaye anakwenda pale anabadilika. Ilinibadili mimi na sitaki kwenda kule tena,” alisema

Pennant alipohojiwa mwaka 2011.
 
Marlon King

Staa wa zamani wa Birmingham na Wigan ambaye alifungwa jela miezi 18 mwaka 2009 baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga mwanamke na kumvunja pua.

King alikuwa katika Baa ya Soho jijini London, Desemba 2008 wakati tukio hilo lilipotokea ambapo alikuwa anasheherekea mkewe kuwa mjamzito huku pia akiwa ametoka kufunga bao la ushindi katika pambano la Ligi Kuu saa chache zilizopita.

Mwaka 2014 alikwenda tena gerezani kwa kifungo cha miezi 18 baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha gari kwa kasi.
 
LUGHA TANO ZA MAPENZI/KUMUONYESHA MTU UNAMPENDA/UNAMTHAMINI:
Kila mtu ana namna yake ya kuweza kutambua kama anapendwa/anathaminiwa,na hii pia inatokana kwa kiasi kikubwa jinsi tulivyolelewa watu hawana mahitaji sawa ,namna ya kuonyeshana thamani inatofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,hivyo ni vyema kujua mahitaji ya mwingine,zifuatazo ni lugha 5 za mapenzi(yes kuonyeshana mnapenda na hii inaenda kwa familia,marafiki,watu unaoshirikiana nao kwa namna moja au nyingine):
 
1.MANENO MAZURI/KUSIFIA /KUPONGEZA:
Kuna watu wanapenda kusikia haya maneno ili waonekane kama wamejaliwa au wanathaminika,maneno haya yanaweza kuwa kusifia tabia,umbile,huduma,muonekano,juhudi
Kuna watu huwa hawajui kusifia,kuwaambia wenzao maneno mazuri kupongeza kwasababu tu wamekulia mazingira ambayo hiyo misamiati kwao haipo,na kuna wengine wamekulia mazingira ya kuambiwa maneno mazur na usipomwambia teyari anaona kuna tatizo,
Hivyo basi tujifunze haya ahsante,umependeza,umefanya kazi vizuri,unavutia,umetoa mada vizuri na mengineyo yanayofanana na maana hii
 
2.KUTUMIA MUDA PAMOJA:
Kuna watu wao kutumia muda pamoja sio muhimu kama ni baba wa familia anaamin kwamba akitoa hela ya matumizi inatosha anaondoka asbh anarud usiku weeken yupo na marafik,hana muda na familia na hata ukimuuliza atakwambia kwan kuna unachokosa,kwake yeye kuhudumia familia inatosha.
Lakin kuna watu bora usimpe hela ya kula lakini upate wasaa wa kuwaangalia kuhakikisha mko salama,kukaa na kusali pamoja,kula pamoja,muda wa mazungumzo na mengineyo.
 
Back
Top Bottom