JUMAMOSI iliyopita, Arsenal ilichapwa 3-1 ilipotia mguu Anfield, Mohamed Salah kapiga mbili, Joel Matip katupia moja, Unai Emery na chama lake wakaandika tena maumivu.
Ni rahisi tu kusema Arsenal ya miaka ya karibuni imekuwa haiiwezi Liverpool wanapokuwa uwanjani Anfield. Mara ya mwisho Arsenal kupata ushindi Anfield ilikuwa Septemba 2012, waliposhinda 2-0, shukrani kwa mabao ya Lukas Podolski na Santi Cazorla, kwenye msimu wa 2012/13 tangu hapo, hawajashinda tena.
Tangu wakati huo, katika kipindi cha miaka saba, mambo mengi sana yametokea, makocha waliokuwa kwenye timu hizo, Brendan Rodgers na Arsene Wenger, wote wameondoka na nafasi zao kuchukuliwa na Jurgen Klopp na Unai Emery.