Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
mhhhhh wamemnukuu vibaya kama selemani matola jaffo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema wananchi walioshambulia msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta, watapewa mkong'oto usiku kucha wa leo na hata wakifa ni sawa tu, maana hata wao walidhamiria kuua.
_
"Ni mkong'oto tu usiku kucha. Kama watakufa sawa tu kwa sababu walidhamiria kumuua Mkuu wa Wilaya, kwahiyo hawa wamechagua kuuawa wao. Na hii sio kinyume cha Haki ya Binadamu. Wao walipaswa kuzifahamu haki za binadamu kwanza kabla hawajampiga DC" amesema Chalamila.
 
Ujumbe wa baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____________________
Mwaka 2015 hatukuchagua malaika kuwa serikali. Tulichagua watu wenye ubinadamu. Watu hao na udhaifu wao wakaunda serikali. Serikali iliyoundwa na binadamu dhaifu, haiwezi kuwa takatifu kama malaika.
Kwa hiyo serikali ni dhaifu, kwa sababu imeundwa na watu dhaifu, na ilichaguliwa na watu dhaifu. Udhaifu maana yake ni "si kamilifu", "si takatifu" na ina uwezekano wa kufanya makosa.

Madaraka hayaondoi udhaifu. Madaraka si chanjo ya kuzuia kufanya makosa.
Kwa hiyo, nafasi au madaraka hayakingi uchoyo, ubabe, ulafi, uwongo, fitna, ukatili, upendeleo, ukabila, udini, ujinga, maradhi, na hila. Kisingizio cha "kufanya siasa" si kinga ya kuzuia madhara ya udhaifu huo.

Hali kadhalika, kutambua udhaifu si tiketi ya kuendelea kufanya makosa.
Kukubali kuwa unaweza kufanya makosa, ni ibada inayokubalika mbele za Mungu kwa sababu ni ukiri (admission) kuwa wewe si Mungu bali mwanadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…