Unajua wapo ambao walianza na wakafika hatua kubwa sana halafu wakapoteza kila kitu lakini wakainuka tena kuanza upya na bado wakafika mbali Zaidi ya walipokuwa mwanzo.
Unaweza ukaja kwangu ukajitetea na sababu mia kwanini umeshindwa kwanini haiwezekani, kwanini ulikata tamaa, lakini mwisho wa siku nitakuuliza maono yako, ndoto zako ni za muhimu kiasi gani kwenye maisha yako?