Hapa utapata habari nzito,(hard news) za hapo kwa hapo, hoja, mahusiano, habari nyepesi nyepesi, udambwidambwi, michezo, burudani, utani, ucheshi.
Pia unaweza kujipatia mke/mume.
Hapa ni mahali tulivu, hakuna povu, wala matusi.
Siasa za kashfa hazina nafasi, wafia dini hawana nafasi, utani usizidi mipaka.
Mitongozo mwisho PM, vinginevyo siri zote zinalindwa na mkuu wa masjala SYB.
Mwisho unapaswa udondoshe likes kwa post zote unazo kutana nazo, likes za hapa huwa hazina macho, kwamba nampa furani kwakuwa ni mshikaji wangu, wala kwamba namnyima furani kwakuwa kanifungia PM[emoji23][emoji23]Likes za hapa hazina hila wala chuki.
Kila unayemuona hapa, ukimkuta kwenye majukwaa mengine mpe likes kwa kila post yake. Waliopo hapa wote ni marafiki zako.
Ikitokea umekwaruzana na mtu hapa unashauriwa uwe na subira.
Vinginevyo soma sana jumbe za jirani myoyambendi zitakusaidia kuishi hapa kwa raha na amani.
Hapa pia kuna anko, huyo anko.....
Kwahiyo humu nikupeana "Likes" tu sio ?