Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukifuata kanuni ya nguvu ya uvutano uhitaji kujua jinsi utakavyofanikiwa. Kazi yako ni kuwaza tu kwa namna inavyotakiwa. Waza na amini kwa asilimia 100. Mengine yote mwachie Mungu au ulimwengu. Mungu pekee ndiye anayekupa njia na bahati, ili wewe ufanikiwe. Atakupa nguvu ya kufanya kazi na ujanja wowote utakaohitajika, katika harakati hizo za mafanikio yako.
 
Ukiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza.

Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.
 
Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.

Uko wapi ubinadamu wa watu?

Ukiwa mgeni katika nyumba ya mtu iache katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta. Ukiazima kitu cha mtu kirudishe katika hali nzuri kuliko ulivyokichukua.
 
Mahakama ya umaskini ni mazingaombwe yanayofanyika katika ulimwengu wa roho kwa sababu, hatuna sheria ya uchawi wala maono. Hata hivyo, hakuna mahakama kama mahakama ya mbinguni.
Mahakama ya umaskini ni uchawi. Uchawi ni mazingaombwe yanayofanyika katika ulimwengu wa roho. Haki haitapatikana gizani, itapatikana nuruni.
 
Kwa hisani ya mkuu wa Masjala SYB
FB_IMG_1567890461908.jpeg
 
Back
Top Bottom