Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Furaha huzuia mkazo (stress)

Mkazo (stress) hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya ki-biology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.
 
Watu wenye furaha hawaumwi mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu

Watu ambao wana mood nzuri wana nafasi nzuri sana ya kuimarisha furaha ambayo huwasaidia kutoumwa homa za mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu tofauti na watu ambao wana mood mbaya.
 
Furaha hurefusha maisha

Watu wenye furaha huweza kuishi kwa miaka 7-10 zaidi tofauti na wasiokuwa na furaha. Katika utafiti uliofanywa kwa wazee 4,000 wa Uingereza wenye umri wa miaka 52-79 ambao walikuwa na furaha mara nyingi zaidi kwa siku na kuonesha kuwa watu wenye furaha walikuwa chini ya 35% kufa ukilinganisha na watu ambao hawakuwa na furaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…