Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ikumbukwe kuna watu wengi sana wako mitaani wakitafuta kazi hivyo ni
muhimu kumshukuru Mungu kama wewe
ni kati ya wateule wake. Ukiwa kazini
mambo mengi hutokea kama
kukwaruzana na Bosi au wafanyakazi
wengine lkn hiyo haipaswi kukunyima raha au kukukatisha tamaa kwani daima
binadamu hatuko sawa na hiyo ilishawahi
kuwatokea watu wengi sana duniani so
usijione kama 'jumba bovu
limekuangukia'.
Ukiwa katika foleni tazama nje utakuta ombaomba wengi hao hawakupenda kua
ombaomba wala hawakuzaliwa hivyo so
tutunze kazi zetu na kuzipenda pia.
 
kwa wale ambao bado wanatafuta kazi
msikate tamaa yaweza kupita muda mrefu
usipate kazi hiyo yaweza kua ni somo ambalo umepewa ili utakapopata kazi
uweze kuithamini, chamsingi ni kusali na
kumwomba Mungu katika yote uyapitiayo.
Remember PRAYER is an essential element
in human survival
 
MAPENZI "Mapenzi yana run dunia" ni kati ya
misemo maarufu duniani kuhusu mapenzi.
Kiukweli uchaguzi wa nani uwe nae ni
muhimu sana katika kukuondolea stress
maishani trust me kama ukichemka hapa
ndo umechemka maishani na utabaki na stress milele so what should you do?
 
Kwanza ni kujitahidi kua na mpenzi
mmoja ambae moyo wako umeridhia kua
nae mtu ambae ukiwa nae unajickia
faraja,mtu ambae mnaendana kifikra na
kiimani ikumbukwe " Love is the spiritual relationship" so spiritually muwe
mnaendana kwani kwa kufanya hivyo
itapunguza stress ktk maisha mana
hakutakua na kupingana katika maamuzi
ya nini kifanyike muda gani.
 
Ladies
20190919_194021.jpeg
 
Stress nyingi huletwa na watu kua na wapenzi wengi na kudhani kama
wanapata 'Total satisfaction' huko ni
kujidanganya hakuna jipya unalolipata
kwa kua na wapenzi tofauti tofauti zaidi
ya magonjwa na kuzidisha stress. 'Kama
huridhishwi na unachokipata zungumza na umpendae ukupatie ili maisha
yaendelee'
 
Pia ni muhimu kutokua na rush
katika swala la ndoa kwani ni muhimu sio
kukimbilia kuoa bali ni kua na uhakika na
huyo unaempa maisha yako awe mwenza
wako. Muhimu pia kumshirikisha Mungu katika uchaguzi wako wa nani uwe nae
kwani mume au mke mwema anatoka
kwa Mungu.
 
FAMILIA Familia ni kiungo muhimu kinachoweza
kukuongezea au kukupunguzia stress hivyo
basi familia inabidi ichukuliwe kwa makini
sana. Familia yatakiwa iwepo kukusuport
na kukushauri lakini usikubali familia
kukuharibia mipango na malengo yako. Ni vizuri kusaidia mambo ya kifamilia lakini
kamwe usiruhusu mambo hayo yachukue
kila furaha uliyonayo maishani.
 
.Ikiwezekana hata
waweza kuwapotezea wanafamilia in the
process of making good life mana mwisho
wa yote utabaki wewe kama mama/baba
wa familia na hao wengine watakua na
familia zao. Vivyo hivyo hata kwa marafiki pia kama
unaona hawakusaidii lolote let them go.
 
Back
Top Bottom