Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Imekuwa ni kawaida kwa vijana kupiga picha na kuziweka kwenye mitandao yao ya kijamaii, lakini hawaishii tu kuziweka na kuacha – bali huhamasisha marafiki zao wazipende (ku-like) na kuwatishia wale ambao huenda hawatazipenda picha hizo kwa kuwaita vilaza na huwa wanasisitiza vilaza pita mbali
 
pia walio-like huwahamasisha wenzao kwenye post zao wawalipe fadhila kwa kusema pita name kwenye ukurasa wangu nimepost u-like picha yangu – huu ndio mchezo kamili wa kulipana fadhila kwa kudanganya ulimwengu kuwa wanapendwa kumbe wanaomba kupendwa.
 
Huu ni kama ugonjwa au uratibu (addiction) wa aina nyingine, huwa unaanza taratibu hatimae inakuwa hatari sana na mtu akizoea muda wote atakuwa anataka aweke kitu na watu wa-like ili apate faraja ama furaha katika moyo wake au waki-share unafurahi zaidi kwa kuwa wamesambaza picha zako ambazo upo sehemu nzuri sana na kuvutia– bila shaka inavutia kama huwa unafanya hivyo.
 
Hali hii ni mbaya kwa sababu inakufanya uwe katika hali mbaya hususani kisaikolojia kwa sababu muda mwingi utakuwa unahitaji kupata mrejesho chanya katika post zako zote utakazo kuwa unaweka katika mitandao yako ya kijamii. Vipi siku usipopata likes nyingi utajihisi nini? Je hutaona kuna kitu kimepungua? Hii hali inashangaza kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…