Upendo huu hupatikana kwa kujifunza, kujiuliza maswali ya msingi, kufanya tafiti na hatimae kupata majibu juu ya tatizo au kitu kinachosumbua au hakikuwa na majibu katika jamii fulani.
Baada ya kupata suluhisho huwa jamii inaweka misingi ambayo imepatikana katika hekima ambazo zitasaidia jamii kuishi vizuri. Leo nimekuandalia njia ya wewe kuishi kifalsafa ambayo itakusaidia kuishi maisha ya mafanikio.
Njia hii ni ‘kujiwekea misingi ambayo utaiishi au kuisimamia katika maisha yako,‘ misingi hii isimamie haswa kwa sababu utakuwa umeichagua wewe mwenyewe hivyo itakuwa ndio njia yako ya kukufikisha katika mafanikio.
Misingi hii ndio itakuwa mapenzi yako yatakayokupelekea wewe kuwa na hekima kwa sababu itakuwa inatatua tatizo la kuwa mtu asie na mafanikio, hivyo hii ni njia itakayokufikisha katika kilele cha mafanikio yale unayoyataka
hichi si kitu cha ajabu kutokea katika dunia hii, hata unaowasikia wamefanikiwa na wao wana misingi ya kifalsafa wanaiishi ndio maana wapo pale walipo kwa kupitia misingi waliojiwekea ipo katika mfumo wa nyanja za maisha ya kila siku tunayoishi, nayo ni kama ifuatavyo;
Kiuchumi – Hapa unatakiwa kuweka misingi maalumu kwa ajili ya kujiinua au kujikwamua kiuchumi. Misingi ambayo itakusaidia kufikia malengo ya kiuchumi kupitia kazi, biashara ama uwekezaji unaofanya
Kiuchumi – Hapa unatakiwa kuweka misingi maalumu kwa ajili ya kujiinua au kujikwamua kiuchumi. Misingi ambayo itakusaidia kufikia malengo ya kiuchumi kupitia kazi, biashara ama uwekezaji unaofanya
Ukishaweka misingi mizuri ya kiuchumi isimamie na usikubali kurudi nyuma cha kufanya ipende na itakupeleka katika mafanikio ambayo ndio hekima ya utatuzi wa tatizo lako ambapo lengo lako ni kuukimbia umaskini.
Kijamii – Hapa unatakiwa kuweka misingi ambayo itakusaidia jinsi ya kuhusiana na wengine. Inahusu uchaguzi wa watu utakaokuwa nao karibu kama marafiki, watu hawa hakikisha wanakuwa na athari chanya kwako ambao watakusaidia kufikia malengo yako.
kumbuka hekima huwa haishindwi, sasa kama utachagua watu wasio sahihi na ukashindwa hapo utakuwa umechagua kutoipenda hekima kwa sababu utakuwa hukufuata hatua za kufikia hekima kwa kujiuliza maswali, kuchunguza na kufahamu wakina nani ni watu sahihi kwangu – kuwa makini hapa!
Pia katika mambo ya kijamii kuna suala la imani, hili suala gumu kwa baadhi kulielewa ila cha msingi hapa weka au chagua imani ambayo unaiamini itakuongoza vizuri kufikia yale ambayo umepanga kuyafikia.
Imani hii iwe inakuruhusu kuhusiana vizuri na wengine hata walio na imani tofauti na wewe. Isije ikawa inakukataza kujumuika na wengine au kuhimiza kuwatenga, mafanikio hayaji kwa kujitenga bali kushirikiana na wengine.
wewe hapo ulipo ni kiungo kimoja ambacho unahitaji kuungana na wengine kama timu moja ili muweze kufanya kitu fulani na kila mmoja akifanya kitu fulani na mkiunganisha matokeo ya kazi au hicho kitu mnakuwa mmefaanikiwa – hapa ndipo hekima kama falsafa huwa imefikiwa kwa kutumia msingi imara wa kijamii.