Kisiasa – Watu tunatofautiana vitu tunavyopenda na malengo pia, inawezekana kuanzia mwanzo sikukugusa kabisa, lakini hapa inawezekana nimekufikisha mahali upapendapo. Ila si lengo langu kujadili sana kuhusu hili ila kwa vile nakufundisha kuhusu misingi ya kifalsafa na hili lipo ndani ya falsafa, sina budi kukufundisha ili ujifunze na kisha ukazidi kutafuta maarifa zaidi juu ya hili. Kama misingi mingine tuliokwishajifunza hapa napo unahitaji kujua wewe kama mpenda siasa una misingi gani katika siasa. Tafuta msingi au misingi unayoweza kuisimamia na ifanyie kazi na itakufikisha katika kile unachokitaka. Hapa ni pagumu wengi huwa wanaanguka kwa kukosa uadilifu, hivyo angalia kwa makini sana misingi unayoweza kuiishi. Kama ni usawa kwa watu wote, kama ni utetezi wa kijinsia au uanaharakati tafuta mahala ambapo ukisimama utakuwa bingwa kwa hekima za falsafa utakazokuwa unatumia jukwaani, umahiri utakulipa kwa kutumia misingi utakayoiishi kwani hiyo ndio itakuwa sifa zako.