Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
tapatalk_1569477500074.jpeg
 
 
Kuhusu Majadiliano na Walio Mahabusu Kwa Kesi za Uhujumu Uchumi, Sheria Inasemaje?

Anaandika Comred Mbwana Camerôò Allyamtu

SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20(CPA)

Sheria hii imefanyiwa marekebisho na sheria ya mabadiliko mbali mbali ya sheria no 4 ya 2019 ( Written laws miscellaneous amendment Act no 4 of 2019. )

Mabadiliko Hayo yameanzisha kitu kinaitwa ikirari majadiliano ( plea bargain).
 
Ikirari majadiliano ( plea bargain) ni majadaliano katika kesi ya jinai Kati ya upande wa mashtaka na mshtakiwa ambapo mshtakiwa atakiri kutenda kosa na kutoa taarifa zinazoweza kuwezesha kuzuia makosa mengine au ili kuharakisha kesi ili aweze kushtakiwa kwa kosa lenye adhabu ndogo Kati ya Mengi au kuondolewa mashtaka au baadhi ya mashtaka.

Upande wa mashtaka na mshtakiwa wakijadiliana na kukubaliana wanaingia mkataba ujulikanao Kama Plea Agreement.
 
Makubaliano yanaweza kuingiwa baada ya Mwendesha mashtaka wa serikali ( Public Prosecutor (PP) ) kushauriana na muathirika wa kosa (Victim) au mpelelezi wa kesi na kuona Kama mazingira yanaruhusu kufanya plea bargain. Na endapo mazingira yanaruhusu muda wowote kabla ya hukumu PP anaweza kufanya Plea burgain na mshtakiwa.

Plea burgain inaweza kuanzishwa na PP, mshtakiwa au Mwanasheria wa mshtakiwa na mahakama lazima ijulishwe.
 
Mahakama haitahusika katika majadiliano Kati ya upande wa mashtaka na mshtakiwa

Matokeo ya majadiliano au makubaliano (Plea agreement) PP anaweza kuamua yafuatayo:-
1. Kumshtaki mtuhumiwa na kosa lenye adhabu ndogo ( offence that attract linient sentence) au kumtolea mashtaka au baadhi ya mashtaka ( withdraw of some counts or the whole charge)
2. PP anaweza kuchukua hatua stahiki kwa kutegemea mazingira ya kesi.
3. PP anaweza kumtaka mshtakiwa kulipa fidia, kurejesha ( restitution) kufilisiwa Mali zote zitokanazo na uhalifu.
Makubaliano (Plea agreement) Kati ya PP na Mshtakiwa lazima yawe katika maandishi na Lugha inayoeleweka na mshtakiwa na lazima yasainiwe na PP na Mshtakiwa pamoja na mkalimani Kama alikuwepo kumtafisiria mshtakiwa.
 
Pia makubaliano lazima yasajiliwe na mahakama na lazima ijilidhishe kuwa yalikuwa ya hiari kwa upande wa mshtakiwa. Na maamuzi Ayo yakikubaliwa mahakama itatoa mahamuzi kupitia makubaliano na maamuzi yakishatoka na mshtakiwa kufungwa, mshtakiwa hawezi kulalamika kuwa kesi yake haikuendeshwa katika misingi ya haki ( fair trial) na hawezi kukata rufaa isipokuwa rufaa ya kupinga kifungo kikubwa tofauti na kosa au rufaa ya kupinga kuwa plea bargain ilikuwa na makosa ( was improperly made)
 
Sheria imekataza kabisa kufanya plea burgain katika baadhi ya makosa yafuatayo:-

- makosa ya kijinsia ( sexual offenses) yenye adhabu zaidi ya miaka mitano au yanayohusisha
mtoto chini ya miaka 18.
-Makosa yanayohusisha uhaini.
- Makosa ya kupatikana na dawa za kulevya zenye thamani zaidi ya million 10.
-Kupatikana na nyara za Serikali zinazozidi thamani ya Tsh million 10.
-Makosa ya Ugaidi au makosa yoyote ambayo Waziri mwenye mamlaka anaweza kuyaongeza.
 
Faida za Plea burgain.
- zinaondoa msongamano wa kesi mahakani na Polisi.
- kurahisisha upelelezi.
-kupata taarifa kupitia wahalifu.
- kupata Mali zilizoibiwa au zilizohusika katika uhalifu kwa urahisi.
- kuwepo kwa mahusiano mazuri Kati ya muathirika, mshtakiwa na PP.

Wajibu wa Mpelelezi.
Mpelelezi anatakiwa kuhakikisha anajua Kama mshtakiwa anahitaji plea bargain na Kama mazingira yanaruhusu anatakiwa kuwasiliana na PP mapema na kumjulisha juu ya hitaji la mshtakiwa la kufanya Plea burgain.
 
Back
Top Bottom