Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Samaki na Yavuyavu (jelly fish)
Jinasue kutoka kwa yavuyavu na kwangua miguu yake ambayo inaweza kuwa imekung’ang’ania. Tumia maji ya bahari kunawa sehemu hiyo. Kwa samaki wanaochoma na miba yao, ondoa miba yote iliyobaki kwenye ngozi kwa kutumia kibanio.

Ingiza sehemu iliyoumia kwenye maji ya moto kwa dakika 20 kupunguza maumivu, lakini hakikisha kuwa hayaunguzi. Hii inaweza kusaidia zaidi kutuliza majeraha kutokana na samaki wanaochoma kuliko yavuyavu.
 
Kuna tiba nyingi za asili lakini siyo zote hufanya kazi dhidi ya madhara ya aina zote za samaki au yavuyavu. Kwa mfano, mashambulizi ya samaki wengine yanaweza kutulizwa kwa kuosha na siki (vinegar). Lakini siki huzidisha madhara ya mashambulio ya aina zingine za yavuyavu. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu v ya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu,. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu vya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu, lakini siyo kwa aina zote za yavuyavu na wakati mwingine vinaweza kuzidisha maumivu.
 
Mhimize atumie na kutembeza viungo vyake —tofauti na matukio ya kung’atwa na nyoka au buibui, kutuliza kiungo bila mtikisiko hakusaidii. Tafuta msaada wa kitabibu kama kutakuwa na matatizo ya kupumua au iwapo dalili zitazidi kuwa mbaya.
 
Kuumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine
Katika sura hii:
Huduma ya kwanza
Weka utulivu na kudhibiti dharura
Kupoteza fahamu (kuzirai)
Kupumua
Pasipo mapigo ya moyo
Kutokwa damu
Mshituko
Vidonda
Vidonda ambavyo vimeingia ndani
Maambukizi
Ueneaji wa sumu ya vimelea kwenye damu (sepsisi)
Tetanasi (pepopunda)
Majeraha ya uti wa mgongo na shingo
Majeraha ya kichwa
Vidonda kwenye kifua na mbavu ambazo zimevunjika
Majeraha na vidonda kwenye tumbo
Mshituko wa moyo
Mifupa iliyovunjika, kutenguka, na misuli au tishu zilizoumia
Kuvia damu kutokana na majeraha chini ya ngozi
Ubakaji
Majeraha ya moto
Kupigwa na umeme
Kuunguzwa na kemikali
Silaha za kipolisi
Dharura zinazohusu afya ya akili
Sumu
Dharura zinazohusiana na ugonjwa wa kisukari
Shambulio linalofanana la kifafa (seizures), mtukutiko wa maungo (convulsions)
Kuumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine
Mzio: Mzio mdogo au mzio mkali
Dharura kutokana na joto kali
Dharura kutokana na baridi kali
Madawa

Usitoboe au kuchana wazi sehemu ulioumwa au kung’atwa au kujaribu kufyonza nje sumu. Pia, toniketi (bandeji au mpira unaofungwa sehemu Fulani ya mwili kudhibiti mzunguko wa damu) hazitasaidia kuzuia sumu kusambaa, lakini zitasababisha madhara mabaya zaidi.
 
Matukio mengi ya kuumwa au kung’atwa na viumbe husababisha maumivu lakini siyo hatari, na hata viumbe hatari kawaida haviachii sumu ya kutosha kuua binadamu. Kuwa mtulivu na tazama sehemu iliyojeruhiwa. Kama hakuna matatizo au matatizo yenyewe yanapungua baada ya saa chache (kutegemea na kiumbe) hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi. Kwa watoto wadogo,hasa kutokana na umri wao, sumu inaweza kuwaathiri na kusababisha madhara makubwa zaidi. Hivyo wanahitaji msaada zaidi na wa haraka.
 
Weka sehemu ya jeraha chini ya usawa wa moyo. Halafu tuliza sehemu ya jeraha kwa kufunga kitambaa cha kuishikilia sehemu yenye jeraha au ubao ili kupunguza kutikisika. Kutumia misuli au kuitembeza huchangia sumu kusambaa.
 
Polepole safisha kidonda. Usipanguse.
Kwa aina nyingi za nyoka, au kama hujui alikuwa nyoka wa aina gani, angalia na kusubiri kwa dakika chache. Kama kuna uvimbe mdogo au hakuna uvimbe wowote, maumivu, au wekundu, hakuna tatizo. Dalili za hatari zinajumwisha kuvimba sana au maumivu makali, kusikia kichwa kizito sawa na mtu anayetoka usingizini, vigubiko vya macho kuinama, kizunguzungu, udhaifu, kichefuchefu, au kutokwa damu puani au mdomoni.
 
Mwambie majeruhi kusukutua maji mdomoni na kutema kwenye bakuli jeupe au lenye uwezo wa kuonesha rangi halisi ya maji yatakayotoka mdomoni. Kama maji yaliyotemwa yataonekana pinki au yenye damudamu, ni dalili kwamba fizi zimeanza kutoa damu. Hii ni dalili ya hatari.
 
Kwa aina ya nyoka wafuatao, funga eneo la jeraha na kukaza:


Nyoka waishio kwenye mawe na matumbawe(coral snakes)
Hongo (mamba)
Nyoka wengi wenye asili ya Amerika ya Kusini
Nyoka wa kwenye maji (sea snakes)
Aina nyingi za Kobra – zenye sumu zinazoathiri mwili mzima.
 
Kwa nyoka wengi wenye sumu, kuna dawa ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti sumu. Kama utapata msaada wa kitabibu, elezea kadri uwezavyo ni nyoka wa aina gani ili dawa sahihi ya kudhibiti sumu ya nyoka iweze kutumika. Kama inawezekana hakikisha una dawa ya sumu ya aina za nyoka wanaopatikana sana eneo lako katika sanduku lako la akiba ya dawa kabla dharura kama hizo hazijatokea.
 
Chatu huwa hawana sumu, lakini wanapong’ata wanaweza kusababisha maambukizi makali ya ngozi. Chunguza kidonda na kama kuna dalili ya maambukizi— wekundu kuongezeka, joto kuongezeka, kuvimba, au usaha, toa matibabu yanayostahili kwa kidonda ambacho kimepata maambukizi. Mara chache nyoka hao husababisha majeraha kwa kujiviringisha juu ya mwili wa mtu na kumkamua.

Kama eneo la jeraha linaonesha meno ya nyoka yalipoingilia, basi nyoka huyu ana sumu. Kama hakuna alama za meno ya nyoka, kuna uwezekano mdogo kwamba nyoka huyu ana sumu, lakini anaweza kuwa na sumu.
 
FB_IMG_1557423204158.jpeg
 
Back
Top Bottom