Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuanza siku vizuri ni ishara ya mafanikio. Je unaanzaje siku vizuri?

Lala vizuri, usingizi wa masaa 6 hadi 8
Pata kifungua kinywa
Oga maji ya uvuguvugu
Kunywa maji mara tu baada ya kuamka
Usifanye mazoezi kabla ya kula
Usiwaze majukumu, anza kwa fikra chanya kila uamkapo
Jaribu kupendeza unavyoweza, na jiamini
 
Chakula cha asubuhi ni muhimu na tumesisitiza sana hili swala kwenye makala zetu nyingi. Kutokana na kutokuwa na mpangilio mzuri wa kufanya maandalizi mapema, wengi wetu hupata uvivu na hata kuepuka kabisa kula chakula hiki muhimu cha asubuhi.
 
Inawezekana ukaona ni swali lisilo na msingi, lakini mara nyingi wengi wetu hatufahamu jinsi ya kupasha moto kiporo. Wengi huweka jikoni na kuwa na papara ya kula kabla hakijapata moto vizuri. Hii si sawa, sababu kila chakula huwa na masharti yake kwenye kupasha moto. Moto husaidia kuamsha virutubisho na vilevile kuua vijidudu vilivyozaliana kwenye chakula.
 
Chakula kikiwa hakijapata vizuri moto hukufanya kujisikia uvivu na hamu ya kulala. Ndio maana mara nyingi watu wengi huingiwa na uvivu na kupenda kulala baada ya kula kiporo kizito cha wali maharage asubuhi. Mie pia imeshanitokea mara nyingi na huwa napenda sana kiporo cha ubwabwa maharage, hasa yakiwa ya nazi
 
Njia nzuri ya kuhakikisha unapasha moto chakula vizuri ni kuwa na microwave. Pasha moto kwa muda usiopungua dakika 4 ili kupata matokeo mazuri. Kama unatumia jiko la kawaida, ni vizuri ukaweka jikoni kwa muda na kuhakikisha chakula kinapata moto vizuri kabla ya kukitenga na kula.
 
Back
Top Bottom