Man United na Fellaini uwanjani ilicheza mechi 176, imeshinda 95, sare 42 na kupoteza mara 39, huku timu ikifunga mabao 283. Man United bila ya huduma ya Fellaini, imecheza mechi 35, imeshinda 14, sare tisa na vichapo 12, huku ikiwa imefunga mabao 42. Kwa wastani, Man United imeshinda asilimia 54 ya mechi zake ilizocheza ikiwa na huduma ya Fellaini na asilimia 40 tu kwenye mechi ilizocheza bila ya huduma ya Fellaini.