Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moyes aliondoka na walipokuja Louis van Gaal na Jose Mourinho wote walimtumia Fellaini katika kusaka matokeo pindi wapinzani wanapoonekana kuwa wagumu, ambapo msimu wa 2014/15 kiungo huyo alifunga mabao saba kuipeleka Man United kwenye Top Four.
 
Kipindi chake, Man United ilikuwa na uhakika wa kupata mabao kutoka kwenye kiungo ya kati, akifunga mara 22 na kuasisti mara 12. Lakini, sasa viungo waliobaki chini ya Ole, Juan Mata, Nemanja Matic, Scott McTominay, Fred na Paul Pogba wote viwango vyao havieleweki, hawana uhakika wa kufunga.
 
Man United na Fellaini uwanjani ilicheza mechi 176, imeshinda 95, sare 42 na kupoteza mara 39, huku timu ikifunga mabao 283. Man United bila ya huduma ya Fellaini, imecheza mechi 35, imeshinda 14, sare tisa na vichapo 12, huku ikiwa imefunga mabao 42. Kwa wastani, Man United imeshinda asilimia 54 ya mechi zake ilizocheza ikiwa na huduma ya Fellaini na asilimia 40 tu kwenye mechi ilizocheza bila ya huduma ya Fellaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…