Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nchini Marekani utumiaji uliopindukia wa panadol (overdose) umetambuliwa kuwa ndio sababu kuu ya simu zinazopigwa kuomba msaada katika vituo vya udhibiti wa sumu (Poison Control Centers) nchini humo, kila mwaka.
 
8EBPtJ3GwvX7tx3GgNEA85-1200-80.png
 
Panadol pia inatuhumiwa kuwa kila mwaka inasababisha kiasi cha watu zaidi ya 56,000 kupatiwa matibabu ya dharura, watu 2,600 kulazwa hospitalini, na kiasi cha watu 458 kupoteza maisha, katika taifa hilo. Sababu ya madhara haya inatajwa kuwa ni kushindwa kwa kiwango cha juu kwa ini kufanya kazi.
 
Taasisi ya chakula na dawa ya Marekani (US Food and Drug Administration (FDA)) mnamo mwaka 2009 ilitoa maelekezo kuwa vifungashio vya dawa hii viwekewe onyo kuhusu uwezekano wa dawa hii kuharibu ini la mtumiaji.
 
Katika hatua nyingine, kwa nia ya kupunguza madhara, mnamo tarehe 14 Januari, 2014 FDA ilitoa kauli iliyokuwa ikiwahimiza wataalamu wa afya kuacha kuandika maagizo ya dawa (prescriptions) kwa dawa mchanganyiko ambazo miongoni mwake kulikuwa na vidonge (au vimiminika) vilivyokuwa na kiambata cha panadol kilichokuwa kikifikia kiasi cha miligramu 325.
 
Ni vizuri kuzingatia kuwa baadhi ya dawa za maumivu zinazotolewa kwa maagizo ya daktari kama vile Vicodin na Percocet, pia zina kiambata cha panadol na kwa hivyo hazipaswi kuchanganywa na dawa zingine zenye kiambata hiki.
 
Back
Top Bottom