Kwenye mechi nane walizocheza Ligi Kuu England msimu huu, Man City wamepoteza mara mbili, wameachwa pointi nane dhidi ya timu inayoshika usukani wa ligi hiyo kwa sasa, Liverpool.
Kinachoelezwa ni kwamba timu kwa sasa zimefahamu namna ya kumkabili Guardiola na kulazimisha atumie kupita pembeni jambo linalowafanya kutumia soka la kupiga krosi zaidi, ambalo hawana ujuzi nalo kwa sana.
Takwimu zinaonyesha kwamba mechi tano za mwisho, Man City imepiga krosi nyingi kuliko wapinzani wao, lakini kitu kibaya zaidi kwenye mechi hiyo, wameshinda moja tu na kupoteza nne zilizobaki.
Wolves waliiduwaza Man City wakati walipowachapa 2-0 uwanjani Etihad, ambapo kwenye mchezo huo, kikosi cha Guardiola kilipiga krosi 27 na hakukuwa na bao lolote.
Kwa kuanzia Desemba, timu ambazo ziliilazimisha Man City kupitia pembeni kwenye mechi zao, ziliwafanya kuwa na wakati mgumu na hatimaye kuibuka na matokeo mazuri ndani ya uwanja.
Kwa kuanzia rekodi za mwanzo wa msimu wa 2018/19, Man City imeruhusu wavu wake kuguswa mara 32 na mara 12 iliyokana na mipira ya kutenga, ikiwa ni wastani wa asilimia 37.5.
Hii inaonyesha kwamba Man City wanapozuiwa tu kucheza soka lao la gonga nyingi na kulazimishwa kucheza krosi, basi mambo yao huwa ya hovyo ndani ya uwanja.
ZINEDINE Zidane atashusha pumzi baada ya mechi iliyotishia usalama wa kibarua chake iliyopaswa kupigwa wiki ijayo huko Nou Camp imepigwa kalenda hadi Desemba.
Kocha huyo wa Real Madrid, Zidane aliripotiwa kwamba huenda akafunguliwa mlango wa kutokea kama angechapwa na mahasimu wao Barcelona kwenye El Clasico, lakini sasa mechi hiyo ya wiki ijayo imeahirishwa hadi Desemba kutokana na vurugu za kisiasa huko Catalunya.
Kocha huyo wa Real Madrid, Zidane aliripotiwa kwamba huenda akafunguliwa mlango wa kutokea kama angechapwa na mahasimu wao Barcelona kwenye El Clasico, lakini sasa mechi hiyo ya wiki ijayo imeahirishwa hadi Desemba kutokana na vurugu za kisiasa huko Catalunya.
Ratiba ya awali ya mechi hiyo ya Nou Camp ilipangwa kupigwa Oktoba 26. Lakini, sasa hukumu ya kifungo kwa viongozi tisa wa siasa huko Catalunya kimesababisha hali ya vurugu kwenye jiji hilo kutokana na maandamano mfululizo jambo linalofanywa mchezo huo kusogezwa mbele.
Uwanja wa Ndege wa Barcelona, El Prat ulifungwa kwa muda Jumanne iliyopita kutokana na vurugu zilizoripotiwa watu 100 kuwekwa kizuizini tangu Jumatatu.
Karibu maofisa 200 wa polisi walijeruhiwa kwenye vurugu hizo na hivyo jambo hilo limewafanya Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) kuamua kupeleka mbele mechi hiyo ya kibabe.
Na sasa kipute hicho kinapangwa kupigwa Desemba 7, lakini kwa Jumamosi hiyo timu hizo zitakuwa na mechi zao za Copa del Rey hivyo nazo zitalazimika kuahirishwa