Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msumbiji, daraja la Samora
FB_IMG_1571486642639.jpeg
 
Mungu ni mkamilifu milele. Anaishi katika ukamilifu wa milele. Hivyo, kabla ya uumbaji, aliishi katika ukamilifu, baada ya uumbaji, ataishi katika ukamilifu.
Ukiichunguza sana hii kauli utajua Mungu ni nani. Mungu ni Muumbaji, aliyekuwepo, aliyepo, na atakayekuwepo.
 
Hapa duniani kuna watu wawili tu: Mungu na wewe! Wengine wote, vingine vyote, wako au viko kisogoni mwako. Nje ya macho yako kuna Nuru. Nuru hiyo ndiye Mungu. Wengine wote, vingine vyote, ni akisi ya taswira ambazo ziko ndani yako; ambazo unatakiwa kuziona nje ili uone umekosea sehemu gani, na uweze kurekebisha dunia yako ya ndani.
 
Yesu ni Mfalme wa wafalme, kwa sababu baada ya muda fulani atarudisha ufalme kwa Baba yake. Mungu ni Mfalme wa milele asiyeweza kuonekana wala asiyeweza kufa, 1 Timotheo 1:17, na haonekani kwa faida yetu wenyewe.

Kwa nini? Kama Mungu yupo, yuko wapi? Kwa nini asijionyeshe ili nasi tumwone? Kama alituumba, kwa nini hatuonani naye uso kwa uso? Kwani tatizo ni nini? Faida ya yeye kutojionyesha kwetu ni nini?
 
Mungu hawezi kujionyesha kwetu kwa kuwa asili yetu ya ubinafsi itasababisha mtafaruku na matatizo makubwa dunia nzima. Kila mtu duniani kote atamng’ang’ania, atamtamani sana, na hakuna la maana litakalofanyika. Itakuwa kinyume na kusudi la maisha; na kusudi la maisha ni kuishi naye mbinguni kwa furaha ya milele, na hatutaweza kuishi naye mbinguni iwapo tuliishi naye duniani.
 
Hewa ipo lakini hatuwezi kuiona wala kuigusa. Hali kadhalika, Mungu yupo lakini hatuwezi kumwona wala kumgusa. Matendo yake makuu kwetu ndiyo yanayofanya tuamini kuwa yupo. Mungu akijionyesha kwetu tutakuwa kama watumwa. Tutakwama ndani ya asili yetu, na hatutaweza kamwe kuwa na upendo.
 
Mungu anasema katika Isaya 66:1, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuwekea miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?” Anasema tena katika Matendo ya Mitume 7:49-50, “
Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana, Au ni mahali gani nitakapostarehe?”
Kulingana na mafungu hayo Mungu ni mkubwa wa kupindukia. Kiwiliwili chake kiko mbinguni, miguu yake iko duniani.
 
Back
Top Bottom