Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umewahi kufikiria hatua aliyopitia mtu huyu? Hivi hakuwa kijana kama wewe? Aliishi maisha ya ujana na alipitia hatua mbalimbali akicheza kama wewe na kupumbazika, akidhani kuwa maisha ya ujana yatabakia hivyo, akidanganyika na nguvu za ujana akazembea katika kutekeleza wajibu wake katika kuyatengeneza maisha ya dunia na Akhera.
 
Baada ya ujana kumtupa mkono, hivi leo amezeeka, udhaifu wa kila namna umeuzunguka mwili wake, maradhi ya aina mbalimbali yanamwandama, sasa analilia fursa ya ujana aliyoipoteza katika mambo ya kipuuzi, na anatamani ujana ungerudi ili atumie nguvu zake katika kufanya ibada.
 
Matumaini ya uongo
Mara nyingi vijana wanakuwa na tamaa nyingi zikiambatana na matumaini yasiyokuwa na ukweli ndani yake. Kijana hutumai kuwa atakapofika katika umri wa utu uzima, miaka 40, atajipinda na ibada pamoja na kutubia kwa Mola wake.
 
Labda tuulizane ni nani mwenye dhamana kuwa atafikia umri wa miaka 30, 40 au 50? Nani mwenye dhamana ya kufika hata kesho? Nani mwenye dhamana kuwa atanyanyuka hapo alipokaa au atafika huko anakokwenda? Umauti hauna taarifa bali huja ghafla kwa kijana, mzee hata mtoto – na sisi wote ni mashahidi kwa wale wenzetu wenye umri kama wetu waliotangulia hali ya kuwa walikuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu.
 
Tujifunze kwa wenzetu. Tujiulize, je waliweza kutubia kabla ya kuondoka kwao? Je katika makaburi yao wameweza kufaidika na yale waliyoyatanguliza katika maisha yao? Kule kupoteza wakati na kujishughulisha na mambo ya kipuuzi kumewanufaisha nini katika hali waliyokuwa nayo hivi sasa? Hawakuweza kuufikia umri waliokuwa wamejipangia wenyewe kwa sabubu jambo hilo halipo katika dhima ya mtu bali mtendaji wa hilo ni Allah peke yake ambaye hahitaji ushauri wa yeyote pindi anapoamua jambo.
 
Epuka neno, ‘Nitafanya’
Jambo lingine ambalo ni kikwazo kikubwa kwa vijana katika kubadilisha mwelekeo wa maisha yao kuwa mzuri ni kitendo cha kutochukua hatua ya mabadiliko papo kwa papo wakawa ni watu wa kusema, “Nitafanya”.
 
Wengi wanasema nitatubu, nitasali, hawasemi nitabadilika. Kauli hii ya kusema nitafanya kadha kwa hakika ni bahari isiyokuwa na mwisho. Waliozama katika bahari hii ni wengi mno. Walikuwa wakisema, nitafanya mpaka wakajikuta wapo ndani ya makaburi.
 
Wengi wanasema nitatubu, nitasali, hawasemi nitabadilika. Kauli hii ya kusema nitafanya kadha kwa hakika ni bahari isiyokuwa na mwisho. Waliozama katika bahari hii ni wengi mno. Walikuwa wakisema, nitafanya mpaka wakajikuta wapo ndani ya makaburi.
 
Back
Top Bottom