Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1227751.jpeg
 
Beetroots hulinda ini
Juisi ya beetroot ina viondoa-sumu (antioxidants), vitamini A, vitamini B-6, na madini ya chuma. Misombo hii inasaidia kulilinda ini dhidi ya uvimbe na msononeko unaotokana na taka sumu (oxidative stress) huku ikimarisha uwezo wake wa kuondoa sumu kutoka mwilini.
 
Anza kwanza kwa kuandaa viazi vyenyewe kama ifuatavyo:
Punguza vichwa vya viazi-sukari kisha vioshe barabara. Usivimenye ili kuwa na virutubisho vingine.
Vikate viazi katika vipande vidogo.
Viweke ndani ya blender, tia maji kiasi kisha saga.
Kunywa juisi iliyopatikana au iweke kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi baadaye.
 
Unaweza kunywa juisi ya beetroot kama ilivyo au waweza kuchanganya na matunda na mboga nyinginezo. Mbogamboga na matunda yafuatayo yanaweza kuchanganywa pamoja na viazi hivi ili kutengeneza juisi murua kabisa:
Matunda ya machungwa
Tufaha
Karoti
Tango
Tangawizi
Nanaa (mint)
Mrehani (basil)
Asali
 
Back
Top Bottom