Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Viazi-sukari kwa kawaida ina madini mengi ya naitrati, ambayo yakiliwa mwili huyageuza kuwa oksidi ya naitriki. Msombo huu husaidia katika kutanua mishipa ya damu, ambayo hupelekea kuboreka kwa mtiririko wa damu na hupunguza shinikizo la damu kwa ujumla.
 
Beetroots hulinda ini
Juisi ya beetroot ina viondoa-sumu (antioxidants), vitamini A, vitamini B-6, na madini ya chuma. Misombo hii inasaidia kulilinda ini dhidi ya uvimbe na msononeko unaotokana na taka sumu (oxidative stress) huku ikimarisha uwezo wake wa kuondoa sumu kutoka mwilini.
 
Anza kwanza kwa kuandaa viazi vyenyewe kama ifuatavyo:
Punguza vichwa vya viazi-sukari kisha vioshe barabara. Usivimenye ili kuwa na virutubisho vingine.
Vikate viazi katika vipande vidogo.
Viweke ndani ya blender, tia maji kiasi kisha saga.
Kunywa juisi iliyopatikana au iweke kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi baadaye.
 
Unaweza kunywa juisi ya beetroot kama ilivyo au waweza kuchanganya na matunda na mboga nyinginezo. Mbogamboga na matunda yafuatayo yanaweza kuchanganywa pamoja na viazi hivi ili kutengeneza juisi murua kabisa:
Matunda ya machungwa
Tufaha
Karoti
Tango
Tangawizi
Nanaa (mint)
Mrehani (basil)
Asali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…