Elena Tambini, Italia
Mwanamke huyu mwenye miaka 26 anasemekana kuvutia watazamaji wengi kwenda uwanjani wanaposikia ndiye atachezesha mchezo. Kwa watazamaji wengi, uzuri wa mwana mama huyu mshika filimbi ndio kivutio chao kikubwa na sio mchezo unaoendelea uwanjani.
Huyu dada ni mrembo na anasifika kwa utaalamu wa kuwapamba wanawake, hasa ma-bi.harusi na wacheza sinema.
Mara nyingi amekuwa muamuzi wa michezo ya Ligi Kuu ya Italia (SerieA) na vilevile ni mchambuzi wa michezo wa kituo kimoja cha runinga.
Wachezaji na mashabiki wengi wanasema mwanamke huyu anavutia kwa sura, mwendo wake wa maringo na sauti nzuri na hata mchezaji ajitahidivipi hujikuta anamuangalia yeye badala ya mpira.