SIKU hizi ni kawaida kuona muamuzi mmoja au wawili wanawake wakichezesha michezo ya kitaifa na ya kimataifa ya soka la wanaume, lakini hutaona mwanamume akifanya hivyo katika mashindano ya wanawake.
Katika mashindano yote makubwa kama ya Kombe la Dunia na ya kanda kama ya Copa America wanakuwapo waamuzi wa kike, lakini sio mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon), ikiwa ni pamoja na yale ya mwaka huu kule Misri.
Au labda wanadhani wachezaji wataelekeza zaidi macho yao kwa kumuangalia muamuzi kama ni mzuri wa sura au kuvutiwa na kitu katika umbile la huyo mwanamama.
Mara kwa mara zimekuwapo simulizi za baadhi ya wachezaji na hata watazamaji wa kandanda kuelekeza zaidi macho yao kuangalia sura na mwenendo wa muamuzi mwanamke anayechezesha kandanda badala ya namna wachezaji wanavyocheza.
Kwa kiasi fulani uzuri wa baadhi ya waamuzi wanawake umesababishaShirikisho la Kandanda la Kimataifa (Fifa) kujikuta na mtihani na kuonekana halijui lianzie au limalizie wapi ili kupata ufumbuzi.
Fifa inataka kukubaliana na baadhi ya wataalamu wa mchezo wa kandanda walioshauri waamuzi wanawake wasichezeshe mchezo wa wanaume, lakini hapo hapo inahofia kuambiwa inafanya ubaguzi.
Katika miaka ya karibuni, baada ya kujitokeza wanawake waamuzi mahiri na wenye beji za Fifa, yapo malalamiko yaliyopelekewa FIFA na vyama, klabu na wachezaji kuhusu ya uzuri unaovutia wa baadhi ya waamuzi wa kike na kutaka wasichezeshe kwa vile huwachanganya wachezaji.

Katika malalamiko hayo inaelezwa kuwa wapo waamuzi wenye kuvutia kupita kiasi na matokeo yake ni badala ya wachezaji kulisakata kabumbu huwa wakati wote wanawakodolea macho kwa matamanio kinamama hao wanaopuliza filimbi au kushika bendera pembezoni mwa uwanja.
Utafiti pia umeonyesha kuwapo watazamaji ambao macho yao huvutiwa zaidi na hao waamuzi na badala ya kufuatilia mpira huwa wakati wote macho yao huwa yamelenga kwa mwanamama anayeshika filimba au kibendera.
Golikipa mmoja wa timu moja ya Amerika ya Kusini ambaye alifungwa bao la kizembe, aliwahi kunukuliwa na gazeti moja akisema alifungwa kwa sababu mpira ulipopigwa macho yake yalikuwa yanaangalia umbo zuri la muamuzi wa kike na sio mpira.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.