Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwao ni waamuzi hawa:
Denise Bueno, Brazil
Mwanamama huyu ambaye sasa ana umri wa miaka 24 mbali ya kuwa ni muamuzi wa kandanda pia ni mrembo anayeshiriki mara nyingi katika mashindanoya mavazi na muziki nchini Brazil.
Ni kawaida kumuona akiwa hajavaa sidiria hata anapochezesha mchezo na huoni chochote kutikisika kifuani kwake anapotembea.
Kinachowaumiza zaidi wachezaji ni pale anapotoa onyo humwambia mchezaji: “Mpenzi huo sio mchezo mzuri’’. Hii kauli ya mchezaji kuitwa mpenzi huwatia mshawasha wachezaji.
 
Fernanda Colombo Uliana, Brazil
Huyu ni muamuzi mwengine mwanamke mwenye kuwafadhaisha wachezaji na watazamaji, ijapokuwa mara nyingi huwa muamuzi msaidizi. Fernanda ambaye sasa ana miaka 29 huwa wakati wote anapochezesha mpira huwa na sura ya tabasamu.
Wachezaji wengi wamethibitisha kwamba hutumia muda mwingi kumuangalia huyu mwanamke anayeshika bendera pembezoni mwa uwanjani badala ya wapi mpira ulipo na mchezo unavyoendelea. Huyu dada naye pia ni mrembo na mchezaji kandanda maarufu.
 
Elena Tambini, Italia
Mwanamke huyu mwenye miaka 26 anasemekana kuvutia watazamaji wengi kwenda uwanjani wanaposikia ndiye atachezesha mchezo. Kwa watazamaji wengi, uzuri wa mwana mama huyu mshika filimbi ndio kivutio chao kikubwa na sio mchezo unaoendelea uwanjani.
Huyu dada ni mrembo na anasifika kwa utaalamu wa kuwapamba wanawake, hasa ma-bi.harusi na wacheza sinema.
Mara nyingi amekuwa muamuzi wa michezo ya Ligi Kuu ya Italia (SerieA) na vilevile ni mchambuzi wa michezo wa kituo kimoja cha runinga.
Wachezaji na mashabiki wengi wanasema mwanamke huyu anavutia kwa sura, mwendo wake wa maringo na sauti nzuri na hata mchezaji ajitahidivipi hujikuta anamuangalia yeye badala ya mpira.
 
Sian Louise Massey-Ellis, England
Mwanamama huyu ana umri wa miaka 33 , lakini ukimuangalia utadhani ana miaka 23 au 24. Ni muamuzi msaidizi wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Naye anatajwa kuwa ni muamuzi anayewachanganya sana wachezaji wa Ligi Kuu ya England na watazamaji kwa uzuri wake na tabasamu yake yenye haiba.
Alichaguliwa muamuzi msaidizi katika mwaka 2010 na baadaye kushiriki kama muamuzi au muamuzi msaidizi katika michezo ya Ligi Kuu ya England.
 
Claudia Romani, Italia
Huyu mwana mama mwenye miaka 35 ni mrembo marufu nchini Italia na nchi jirani na hazipiti siku mbili au tatu bila ya habari na picha zake kutumika katika magazeti ya Italia.
Mwana mama huyu anazungumzwa kama mwanamke anayependa mahaba na kutembelea sana maeneo ya starehe na akiingia katika klabu ya disco basi hubaki humo kucheza muziki mpaka asubuhi. Mara nyingi huchezesha michezo ya Serie A na Serie B ya ligi ya Italia.
 
Muargentina huyo alifunga bao la kuongoza kwenye ushindi wa 2-1 iliyopata Barcelonna mbele ya Slavia Prague na hivyo kujiweka sawa kwenye Kundi F. Slavia Prague walipambana kuchomoa bao hilo, lakini baadaye shuti la Luis Suarez lilimbabatiza winga wa Slavia, Peter Olayinka na kujifunga jambo lililomfanya Messi na kikosi chake cha Barcelona kuondoka uwanjani na ushindi.
 
Na tangu wakati huo amekuwa akifunga walau bao moja katika kila msimu hadi sasa, huku ubingwa wa taji hilo alibeba mwaka 2006 dhidi ya Arsenal. Akabeba pia mara mbili, 2009 na 2011, mara zote alicheza fainali dhidi ya Manchester United. Taji lake la nne la ubingwa wa Ulaya, alilibeba mwaka 2015 kwenye fainali dhidi ya Juventus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…