Akiibukia kwenye timu akiwa na umri wa miaka 16 tu, Wayne Rooney alipata dili la kwenda kujiunga na Manchester United na hivyo kuachana na Everton iliyomkuza na kumuibua. Baada ya kucheza miaka kibao huko Old Trafford, mwaka 2017 akiwa tayari ameshavuka umri wa miaka 30, Rooney aliamua kurudi zake kujiunga na timu yake ya utotoni, Everton alipoachana na Man United. Kinara huyo wa mabao wa muda wote kwenye kikosi cha Man United na England, aliona si kitu zaidi ya kurudi kwenye timu yake hiyo ya utotoni kabla ya kupata dili la kwenda kujiunga na soka la Marekani. Aliporudi Everton, alitumika zaidi kwenye kiungo na kufunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu England.