Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini hilo la uwanamapinduzi halionekani kwenye haiba yake mpaka kwanza ‘apige maji’ na yamtoshe. Mara tu akishalewa chakari, hapo ndipo Mandola Mwanamapinduzi huibuka ndani yake. Yule tajiri mlafi anayetaka kukigeuza kijiji kizima kilichopewa jina lake kuwa eneo huru la kiuchumi na kuwafukuza kwa dhuluma wakulima wa kijiji hicho, hutoweka.
 
Lakini wakati wanakijiji wameshahamasika, mwenyewe anapitia mlango wa nyuma wa kasri lake, ambako kwa bahati mbaya anatumbukia kwenye bwawa la maji na hivyo ulevi unamtoka na sasa Mandola tajiri mlafi anaibuka ndani yake. Anachukua bunduki na kuwaelekeza wanakijiji wanaoelekea kulivamia kasri lake kutwaa haki yao kwa njia ya mapinduzi ya umma.
 
Wanakijiji wote wanakimbia, huku wakijiuliza: “Lakini sini huyu huyu aliyetuhamasisha tufanye mapinduzi tukatwae haki zetu kwake sasa hivi tu!?” Kisha Bwana Mandola anamgeukia dereva wake, Matru, na kumuuliza kwa nini amemruhusu (yeye Mandola) alewe mpaka kupitiliza, ilhali anajua kuwa tajiri wake huyo akishalewa hupoteza fahamu na kuwa Mandola mwengine.
 
Kinapokuwa‘kizima’ hakijalewa, ni chama kilichoshika dola na hatamu za uongozi na chenye ulafi wa kutosha kuhalalisha upapiaji wake wa madaraka. Kimefanya hivyo miaka nenda miaka rudi kwa jina la kukubalika na umma kwa mbinu na kiwango kile kile Bwana Mandola anachofanya kwenye umiliki wa ardhi ya wanakijiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…