Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ghilba, jeuri na kiburi, kwa kushirikiana na mawakala wake waliomo kwenye asasi na taasisi kilichoziunda chenyewe kutoka unyayo hadi utosi wa nchi.

Lakini CCM ina khulka ya ulevi. Kwa hakika imeshalewa na kulewalewa kwenye madaraka, kiasi cha kwamba baadhi ya wakati andasa za kilevi hupanda kichwani zikaiibua CCM nyengine ndani yake – taasisi ya kimapinduzi hasa kama lilivyo jina lake.
 
Kipindi cha mwaka mmoja uliopita andasa hii ya CCM ikampanda mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye naye akadhukuru “matarajio ya kimapinduzi” kwa kutangaza mchakato wa kuelekea katiba mpya. Ilikuwa andasa ya kilevi ya Bwana Mandola, maana nani asiyejua kuwa miezi michache tu kabla ya hapo CCM hiyo hiyo ilikuwa imeng’ang’ania kuwa katiba iliyopo ‘yatosha’?
 
Lakini Rais Kikwete akazuka ghafla-bin-vuu akisema vyengine – kwamba katiba hii haitoshi. Panapaswa kuwepo na nyengine. Nchi nzima ikainuka kumpigia makofi na kumpongeza. Bwana Mandola akatunga wimbo na ngoma ya kimapinduzi. Mapinduzi hupinduliwa mtawala. Mtawala hapa ni CCM. Hivyo wimbo wa katiba mpya ulikuwa ni wimbo wa kuipindua CCM. Ikateuliwa Tume ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba (pia mwana-CCM) kuusimamia mchakato huo.
 
Kumbe Jaji Warioba na wenziwe walikuwa na jukumu la ‘kumdhibiti’ Bwana Mandola asilewe, ama akilewa asipitilize. Haikufanya hivyo. Ikauwacha wimbo wa kimapinduzi kwa jina la katiba mpya ulioanzishwa na mwenyekiti mwenyewe wa CCM usikike, uakisike na mwangwi wake uaminike kwa umma.
 
Tangu hapo, Bwana Mandola ndani ya CCM amekuja juu kama moto wa kifuu. Hakuna tusi alilowachwa kutukanwa Jaji Warioba na wenzake kwenye Tume kwa kuja na pendekezo hilo. Na hata ilipodhihirika wazi kwamba wananchi walio wengi kupitia ama kauli zao za moja kwa moja au kupitia vyama vya siasa, makundi ya kijamii au asasi za kiraia zinazowawakilisha, wanaunga mkono pendekezo la Muundo huo wa Muungano, CCM haikuacha kufanya mbinu na hila.
 
MK14
FB_IMG_1572029010781.jpeg
 
Na mie na hofu maisha yake kuwa akifika kule hatoweza kupata salama. Kwanza kuwa yeye amefikia kwangu, anajulikana yeye na mimi ni rafiki, Nyerere atajua zaidi/uzuri hayo kuwa mimi tangu tuko kule tunasikilizana mimi na ndugu huyu Abdallah. Kwa hali hiyo mimi namwambia. Na yeye Abdallah anasema hana ugomvi na Nyerere.
 
Sasa mimi nimekwiteni mzungumze naye, mseme naye. Akatuchukua akatupeleka kwenye chumba akasema; “Abdallah, hebu zungumza nao hawa jamaa wamekuja kukuamkia.” Tukaingia sie chumbani akatuacha mimi na Ahmed [Rajab] na Abdallah. Peke yetu watu watatu. Ndivyo ninavyokumbuka mie na ndivyo anavyokumbuka Ahmed [Rajab].
 
Mimi sikumbuki ile nilikwenda railway station. Kile mimi sijakumbuka. Kama ulivyosema, mimi nyumba nilikuwa naijua, sina haja ya Kasembe kunpeleka. Lakini inaweza kuwa nimekwenda mimi na Kasembe kumpokea Ahmed Rajab. Yeye Ahmed kafkiri tu na mie ni mgeni. Hajajua kuwa mimi na Kambona tunajuana na jirani, na nyumba yangu mie na yake si mbali.
 
Back
Top Bottom