Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilishtuka sana. Mimi ni Mzanzibari na nilijuana na Hanga kwa miaka mingi na nilikuwa nasikia mengi. Hanga alipofika nilikwenda kumlaki na tukatoka sote nje ya uwanja na hapo nikamualika yeye na mkewe chakula cha mchana hapo hapo uwanja wa ndege.
Wakati tunatoka nje ya uwanja nilimuuliza Hanga iweje karejea nchini wakati kama ule. Hanga akanijibu kuwa hapana kitu. Mimi sikuridhika.
 
Tulipomaliza kula na tukawa tanazungumza nilitaka kwa mara nyingine niufungue moyo wangu kwa Hanga. Sikumbuki nilifanya nini lakini niliweza kumtoa mkewe pale mezani tukabaki sie wawili, mimi na Hanga. Hapo nikamwambia Hanga kuwa ni vyema kama akirejea London na ndege ile ile aliyokuja nayo. Hanga hakunisikiliza.
 
Picha hii iliyochukuliwa tarehe 16 Januari 1968 inamuonesha Mwalimu Julius Nyerere akihutubia mkutano wa kumuumbua Abdullah Kassim Hanga (aliyekaa baina ya maaskari wawili) na hiyo inaaminika kuwa siku ya mwisho Hanga kuonekana hadharani.
1572030542688.png
 
Msiba mkubwa wa historia za viongozi wa Afrika ni kuwa wao hutaka historia ziandikwe zitakazowakweza wao na si kinyume cha hivyo. Historia ya Zanzibar haikusalimika na tatizo hili. Hadi kilipotoka kitabu cha Dr. Harith Ghassany, “Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,” historia ya mapinduzi yaliegemezwa katika ujuzi wa mipango ya ASP na Makomredi wa Umma Party. Historia ikisema kuwa hawa ndiyo waliofanikisha mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964
 
Ikiwa tutafunua picha nyingine kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na mikono mingi itabidi tuitafute hii mikono imetoka wapi. Hapa ndipo anapoingia Dr. Harith Ghassany na utafiti wake uliompitisha maktaba nyingi Marekani na Uingereza na mwisho kuishia katika mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi, Tanga. Hapa ndipo lilipotoka jeshi la Wamakonde waliovushwa hadi Zanzibar na kusaidia katika mapinduzi. Katika mashamba haya ya mkonge ndipo anapoingia Abdallah Kassim Hanga.
 
Jeshi lile lilikuwa katika ardhi ya Tanganyika huru na kiongozi wa Tanganyika anafahamika kuwa ni Julius Kambarage Nyerere. Iweje nchini kwake liwepo jeshi ambalo lilivuka mikapa ya nchi yake kwenda kushiriki katika kuvamia nchi jirani. Hapa ndipo unapokutana na Abdallah Kassim Hanga na Oscar Kambona.
 
Back
Top Bottom