Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

William Gallas, 2007-2008

Beki huyo Mfaransa, Gallas kwanza ameweka rekodi ya aina yake kwa kucheza katika klabu pinzani za jiji la London, Arsenal, Tottenham na Chelsea katika kipindi chake cha miaka 12 aliyocheza soka England. Kwenye kikosi cha Arsenal alichaguliwa kuwa nahodha kitu ambacho mashabiki hawajakiunga mkono kabisa wakiamini Gilberto Silva alistahili jambo hilo lakini Arsene Wenger alimpotezea tu.
 
Gallas alikosolewa uongozi wake wa ndani ya uwanja kwenye mechi dhidi ya Birmingham City ambapo straika wa Arsenal, Eduardo alivunjika mguu. Baada alivuliwa kitambaa hicho cha unahodha baada ya kuwakosoa wachezaji wenzake hadharani kwamba wamekuwa goigoi, hawapambani kushinda mataji.
 
Cesc Fabregas, 2008-2011

Kulikuwa na maswali kama Cesc Fabregas alikuwa na viwango vilivyostahili kupewa unahodha kwenye kikosi cha Arsenal. Fab alikuwa kwenye kiwango bora kabisa na hakika alionekana nahodha mzuri katika kikosi hicho cha kocha Wenger. Alionekana kama anapita kwenye nyayo za Patrick Vieira. Lakini, baadaye, Fabregas alikwenda kuwakata maini mashabiki wa Arsenal baada ya kulazimisha kurudi kwenye klabu yake ya utotoni, Barcelona. Arsenal walifanya jitihada zote abaki, lakini Fabregas hakujali yeye ni nahodha aliamua kuingia hadi kwenye mgomo ili kushinikiza kuhamia Barcelona na hata kukubali mshahara wake ukatwe kulipia baadhi ya ada ili tu aachane na Arsenal.
 
Robin van Persie, 2011-2012

Baada ya kukasirishwa na namna Cesc Fabregas alivyoonda kwenye kikosi chake, kocha Wenger alimgeukia straika Robin van Persie na kumfanya kuwa nahodha wake. Fowadi huyo wa Kidachi alikabiliwa na majeruhi mengi sanna mwanzoni mwa miska yake kwenye klabu hiyo, lakini baadaye alitulia na kucheza soka la aina yake. Alifunga mabao 30 kwenye Ligi Kuu England akiwa amevaa kitambaa cha unahodha, lakini ghafla mambo yakaanza kuhusu mpango wa kutaka kuachana na timu hiyo.
 
Thomas Vermaelen, 2012-2014

Wakati Vermaelen alipokuwa beki wa kati kwenye kikosi cha Arsenal kilionekana kuwa ni kitu kisichotumia akili wakati alipokabidhiwa kitambaa cha unahodha wa timu hiyo. Mambo hayakuwa matamu na Mbelgiji huyo mambo yalianza kuchacha kiasi cha kumfanya kocha Arsene Wenger kumpiga chini kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich. Majeruhi yalianza kumtibulia mambo yake beki huyo na kuishia kucheza mechi 14 za ligi kwenye msimu wake wa mwisho klabuni hapo. Hakutumika kwenye fainali ya Kombe la FA mwaka 2014 na baada ya hapo haikumchukua muda akaamua kutimkia zake Barcelona.
 
Mikel Arteta, 2014-2016

Tofauti na wengine kwenye orodha hii, kiungo huyo maarufu alijitengenezea jina lake na kuwa kiongozi shupavu kwenye kikosi hicho cha Emirates. Lakini, shida ilikuwa majeruhi ya mara kwa mara. Mhispaniola huyo alicheza mechi 16 tu za ligi kwa miaka yake miwili aliyokuwa nahodha wa Arsenal. Arteta alikuwa na akili ya mpira kiasi hadi ilifika wakati alihusishwa na mpango wa kumrithi kocha Arsene Wenger mwaka 2018 baada ya kuonyesha mafanikio makubwa huko Manchester City akiwa msaidizi wa kocha Pep Guardiola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…