Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rekodi ya kukosa penalti nyingi ndani ya msimu mmoja mpaka sasa inashikiliwa na timu za Liverpool na Tottenham ambazo zote zimewahi kukosa penalti tano ndani ya msimu mmoja. Katika msimu wa 1994/95 Tottenham walikosa penalti tano msimu mzima wakati msimu wa 2011/12 Liverpool walikosa penalti tano.
 
Kocha huyo kutoka Norway aliamua kumteua mshambuliaji, Marcus Rashford kuwa mpigaji wa penalti za United, lakini mechi iliyofuata tu staa huyo wa kimataifa wa England alikosa penalti muhimu katika pambano dhidi ya Crystal Palace huku United wakichapwa mabao 2-1 nyumbani Old Trafford.
 
FB_IMG_15487363060340213.jpeg
 
Tayari Rashford alikuwa amepigiwa upatu kupiga penalti hiyo baada ya kufunga penalti yake katika pambano la ufunguzi dhidi ya Chelsea ambapo United walishindwa mabao 4-0 nyumbani, lakini pia msimu uliopita alipiga penalti ya bao pekee la ushindi katika pambano dhidi ya Leicester City nyumbani.
 
Katika pambano hili la Norwich, kikosi cha United kilionekana kuwa na hamu ya kupata matokeo baada ya kufuunga bao la mapema kupitia kwa kiungo wa kimataifa wa Scotland, Scott McTominay na baada ya muda mfupi United walipata penalti baada ya kinda wao mahiri, Daniel James kuchezewa madhambi na mlinzi, Ben Godfrey.
 
Rashford alijitokeza kupiga penalti hiyo lakini Krul aliicheza katika upande wake wa kulia. Kipa huyu wa Uholanzi anaonekana kuwa mtaalamu wa kudaka penalti baada ya kuingizwa katika dakika za mwisho na kocha, Louis van Gaal katika pambano la kombe la dunia 2014 dhidi ya Costa Rica nchini Brazil na kucheza penalti.
 
Kipa huyo ambaye alikuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Jasper Cillessen baada ya dakika 120 alidaka penalti mbili ambazo ziliipeleka Uholanzi katika hatua ya nusu fainali ambapo walitolewa na Argentina ambayo ilitinga fainali na kuchapwa bao 1-0 na Ujerumani.
 
Krul pia aliicheza penalti ya Martial ambayo aliamua kupiga upande mwingine tofauti na ule wa Rashford, lakini bado kipa huyo wa zamani wa Newcastle United akagundua ujanja wake na kuucheza mpira akithibitisha ubora wake katika mikwaju ya penalti. Japo kwenye mchezo huo Rashford na Martial wote walifunga bao.
 
Back
Top Bottom