Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Mane kushutumiwa kujiangusha katika eneo la hatari kwa ajili ya kupata penalti. Staa wa zamani wa England, Alan Shearer ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, alimtuhumu Mane kwa kujiangusha katika pambano la Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace hivi karibuni.
 
Sidhani kama ni penalti, amejiangusha tu. Soka ni mchezo wa kugusana. Mane amejigusisha kwa (Marc) Albrighton na ameamua kwenda chini,” alilalamika Shearer mara baada ya kumalizika kwa pambano dhidi ya Palace ambapo Liverpool walipata penalti katika dakika ya mwisho iliyofungwa na James Milner.
 
Griez angebaki tu atleko kwanza hapo tayari ana world kap angerithika tu na hilo kombe kuliko kujipeleka asipotakiwa kisa kikombe cha la liga na ucl
Mwenyewe tu alipishana na muda yaani Muda Barca wanamuhitaji kama unakumbuka alileta pozi na dharau hivyo aliwakera waanazi wa Barca wakamfugia chuki, muda kalegeza na kujileta watu walishamkunjia Roho kitambo ndio maana ata hakukua na utambulisho wake.
 
Pambano kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City linatazamiwa kuzua vita kubwa ya maneno kutokana na upinzani mkubwa uliojengeka baina ya timu hizo hasa kuanzia msimu uliopita ambapo City waliutwaa ubingwa wa England kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Liverpool.
 
Mpaka sasa Liverpool wanaongoza Ligi kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya City huku wakiwa na pointi 31 wakati City wana pointi 25 baada ya kupoteza mechi mbili na kutoka sare moja huku Liverpool wakiwa wametoka sare moja tu dhidi ya Manchester United.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…