Zifuatazo ni baadhi ya dawa zinazo ingiliana (interact) na albendazole :
• Cimetidine, dexamethasone au praziquantel dawa hizi huangeza madhara (side effects) za albendazole.
Huu sio muingiliano pekee unaoweza kutokea kama mtu atatumia albendazole pamoja na dawa zingine. Upo muingiliano mwingi. Wasiliana na mtaalam wako wa afya kabla haujaanza, haujasimamisha au kubadili dozi ya dawa yako yeyote ile.
Matumizi Sahihi ya Albendazole
Tumia kama ulivyoelekezwa na daktari wako. Angalia kwenye lebo ya dawa yako kwa ajili ya maelezo zaidi.
• Tumia kwa njia ya mdomo kama unashindwa kumeza kidonge kizima, unaweza kukitafuna kwanza kasha kumeza na maji kidogo.
Kama ukisahau kumeza dozi moja kwa muda muafaka, jitahidi kunywa kabla muda haujapita zaidi. Kama muda wa kunywa dozi nyingine umefika, endelea na dozi nyingine kama kawaida, usinywe dozi mbili kwa mara moja. Kama umesahau kunywa zaidi ya dozi moja, wasiliana na daktari au mfamasia wako.
Albendazole inabidi zitumike kwa uangalifu mkubwa kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja kutokana na kuwa usalama wa dawa hizi kwa kundi hili la watoto bado haujafhamika vizuri.
Usitumie albendazole kama una ujauzito au unanyonyesha. Albendazole zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto aliyepo tumboni. Bado hakuna majibu ya moja kwa moja kama albendazole huteza kupenya na kuingia kwenye maziwa ya mama anenyonyesha. Na ikiwa utatumia dawa hii na unaujauzito wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.