Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

D84F36DD-D94A-445D-B038-9FE89C052ADF.jpeg
 
Kijamii – Hapa unatakiwa kuweka misingi ambayo itakusaidia jinsi ya kuhusiana na wengine. Inahusu uchaguzi wa watu utakaokuwa nao karibu kama marafiki, watu hawa hakikisha wanakuwa na athari chanya kwako ambao watakusaidia kufikia malengo yako. kumbuka hekima huwa haishindwi, sasa kama utachagua watu wasio sahihi na ukashindwa hapo utakuwa umechagua kutoipenda hekima kwa sababu utakuwa hukufuata hatua za kufikia hekima kwa kujiuliza maswali, kuchunguza na kufahamu wakina nani ni watu sahihi kwangu – kuwa makini hapa!
 
Pia katika mambo ya kijamii kuna suala la imani, hili suala gumu kwa baadhi kulielewa ila cha msingi hapa weka au chagua imani ambayo unaiamini itakuongoza vizuri kufikia yale ambayo umepanga kuyafikia. Imani hii iwe inakuruhusu kuhusiana vizuri na wengine hata walio na imani tofauti na wewe. Isije ikawa inakukataza kujumuika na wengine au kuhimiza kuwatenga, mafanikio hayaji kwa kujitenga bali kushirikiana na wengine. wewe hapo ulipo ni kiungo kimoja ambacho unahitaji kuungana na wengine kama timu moja ili muweze kufanya kitu fulani na kila mmoja akifanya kitu fulani na mkiunganisha matokeo ya kazi au hicho kitu mnakuwa mmefaanikiwa – hapa ndipo hekima kama falsafa huwa imefikiwa kwa kutumia msingi imara wa kijamii.
 
Kiutamaduni – Weka msingi ambao utakuwezesha kuishi tamaduni bora na yenye tija kwa maendeleo, yenye kukuhamasisha kujifunza zaidi juu ya maendeleo. Ile tamaduni ambayo haina faida zaidi ya kukurudisha nyuma achana nayo mara moja hata kama ulizaliwa nayo na badala yake jifunze nzuri na mpya. Kama zama hizi za sasa inabidi ujifunze zaidi kuhusu tamaduni zenye tija.
 
nadhani unatambua kuwa moja ya kiambata cha utamaduni ni lugha, hivyo ikiwezekana jifunze lugha ata mbili au tatu hususani za kimataifa ili uweze kujifunza vitu vingine kwa mapana hata kama vipo katika lugha tofauti na ya kwako – kumbuka kupata maarifa ndio msingi muhimu wa kufikia hekima ya kifalsafa, sasa kwa nini ukose maarifa kwa kufungwa na lugha? jifunze zaidi.
 
Kisiasa – Watu tunatofautiana vitu tunavyopenda na malengo pia, inawezekana kuanzia mwanzo sikukugusa kabisa, lakini hapa inawezekana nimekufikisha mahali upapendapo. Ila si lengo langu kujadili sana kuhusu hili ila kwa vile nakufundisha kuhusu misingi ya kifalsafa na hili lipo ndani ya falsafa, sina budi kukufundisha ili ujifunze na kisha ukazidi kutafuta maarifa zaidi juu ya hili.
 
Back
Top Bottom