Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sare ya 1-1 ya wikiendi iliyopita dhidi ya Wolves uwanjani Emirates imemweka kocha Emery kwenye matatizo makubwa ya kuhusu usalama wa kibarua chake huko Arsenal, kwamba huenda akafunguliwa mlango wa kutokea na tayari makocha kibao wanahusishwa na kazi hiyo.
 
5.Patrick Vieira
Gwiji huyo wa Arsenal bila ya shaka ndoto zake ni kwenda kuinoa timu hiyo siku moja. Lakini, Vieira atahitaji kujiweka fiti kwanza mwenyewe kabla ya kuvamia kibarua hicho cha kuinoa Arsenal, la sivyo mambo yatamwendea kombo na kuondoshwa kwa aibu. Kibarua chake cha huko Nice hakijaenda sawa. Vieira atahitaji kupita kwenye njia anazopita kiungo mwenzake wa zamani, Frank Lampard ambaye amerudi kuinoa klabu yake ya zamani ya Chelsea na mambo yake si mabaya Stamford Bridge.
 
Ilionekana kama ni kitu kinachokwenda kutokea, Mikel Arteta alipohusishwa na mpango wa kurithi mikoba ya Wenger mwaka 2018, lakini mabosi wa Arsenal waliamua kwenda kunasa huduma ya Emery.
Arteta, ambaye ni kiungo wa zamani wa Arsenal, kwa sasa ni kocha msaidizi wa Pep Guardiola huko Manchester City na wamekuwa na mafanikio makubwa kwa misimu mitatu sasa, wakifanikiwa kubeba tu mataji ya ligi za ndani. Guardiola alionekana kukubali wazo la Arteta kwenda kuchukua mikoba ya Wenger ilipoonekana kuwa hivyo na sasa anapewa nafasi upya kabisa.
 
3.Brendan Rodgers
Leicester City wamekuwa kwenye moto kwelikweli kwa sasa kitu ambacho mashabiki wa Arsenal wanatamani hiyo ingekuwa timu yao. Kocha Rodgers anaonekana kufahamu namna nzuri ya kutumia wachezaji kwenye kikosi chake na kuifanya Leicester City kuwa kwenye timu tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England.
 
Mashabiki wa Arsenal wanataka soka la kushambulia, lakini pia wakiwa na beki imara, kitu ambacho ndicho wanachokifanya Leicester City ya Rodgers na kumfanya kocha huyo wa zamani wa Liverpool kutajwa kwenye orodha ya wanaoweza kutua Arsenal.
 
Back
Top Bottom