Mkazi wa Kijiji cha Kowak Wilayani Rorya Mkoani Mara, Juma Olemo amekutwa amejinyonga hadi kufa katika nyumba ya kulala wageni Tarime na kuacha ujumbe wa barua yenye kurasa mbili akiwataka Rafiki zake kuachana na waganga wa kienyeji wapotoshaji.
_
Akisoma ujumbe ulioandikwa katika barua hiyo kwa Wanahabari Kamanda wa Polisi Tarime- Rorya, Herry Mwaibambe amesema Olemo ameomba msamaha kwa uamuzi aliochukua na kuwaasa Vijana wenzake kuachana na waganga wa kienyeji wenye kujihusisha na mambo ya kishirikina na kuwaaminisha kuwa watabadili maisha yao kwa ushirikina na kupata fedha.
_
Kamanda Mwaibambe amesema katika barua hiyo Olemo amewataka Rafiki zake siku ya mazishi yake wacheze mpira wa miguu ili kumuaga, pia amewaomba msamaha mashabiki wa Klabu ya Simba Nchi nzima kwa uamuzi wake huo wa kujinyonga na pia amewaomba msamaha waendesha bodaboda na kuwaasa kufanya kazi halali na kutowaamini waganga wa kienyeji .
_
Katika barua hiyo amemtaja pia Mkewe na kumuomba msamaha kwa kujinyonga na kumuomba Mdogo wake kumtunza Mke na Watoto wake.
#MillardAyoUPDATES