Vile maisha na pesa ilivyongumu kipindi hiki.
Halafu na sikukuu zinakaribia,kuna kulipa ada na kodi then unaletewa habari kama hizi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]unaweza kuwa chizi walah.
Pesa zinapoteaje?39m??kirahisi tu??[emoji23][emoji23][emoji23]woooiii
***********************************************[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Sherehe za kugawana faida katika kikundi cha ujasiriamali cha ‘IMANI’ chenye Makao Makuu yake Ngusero Arusha, zimegeuka majanga na vilio kwa Wanachama na wengine kuzimia ghafla ukumbini baada ya taarifa ya upotevu wa Tsh. Million 39 zinazodaiwa kuyeyuka kwa njia za ushirikina .
_
Fedha hizo ziliyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa Mweka hazina wa kikundi hicho chenye watu 20, kikundi kina miaka 5 na hawajawahi kugawana faida kwa miaka yote hadi juzi walipokaa na kukubaliana kugawana faida.
_
Wanawake waliokuwa wameambatana na Waume zao ili kupokea gawio kwa lengo la kufanya manunuzi na mahitaji mengine majumbani walishikwa na butwaa baada ya kuambiwa fedha zimeyuka kwa ushirikina maana sanduku halijavunjwa, Katibu wa kikundi amesema Viongozi watakutana kujua tatizo kiundani ili watoe taarifa Kamili.
#MillardAyoUPDATES