''Ni kazi ngumu'', anasema Ric Brewer ambae ni mmiliki wa shamba jingine la konokono huko Washington.
''USDA inapanua vitendea kazi, wakaguzi wa kupitia mashamba ya konokono''anasema Brewer
Shamba lake lilifunguliwa mwaka 2011 na sasa lina konokono 50,000, na wengi wao ni aina ya wale wadogo wadogo.
''Ni chakula kizuri sana na hawana madhara kwenye mazingira, na wanapikwa kama ambavyo ungepika dagaa kamba ama kaa'' anaongeza Brewer.