Huu ni ugonjwa wa akili kabisa,its so sad[emoji24][emoji24][emoji24]
-------------------------------------------
Mkazi wa Kijiji cha Mavanga Ludewa Mkoani Njombe Christina Mlelwa mwenye umri wa miaka 38 anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za Kumuua Mtoto wake Joseph Gumbilo mwenye umri wa miaka minne, Mtoto huyo alikuwa mlemavu ambaye hawezi kutembea zaidi ya kutambaa tu.
_
Inadaiwa Christina alimchinja Mwanae na kisha kumla nyama kwa kuvipika viungo vya Mtoto huyo huku akidaiwa kuitupa mifupa kwenye choo kilichopo jirani na nyumba anayoishi.
_
Akihojiwa na Mkuu wa Mkoa Ole Sendeka Mwanamke huyo ambaye alikua akiongea kilugha na Mkazi mmoja kusadia kutafsiri amekiri kutekeleza mauaji ya Mwanae kwasababu alikuwa na ugomvi na Mume wake ndipo alipopandwa na hasira na kuamua kumkaba Mtoto wake na kufanya ukatili huo.
_
"Tunamuuliza Mtoto yuko wapi anasema amemchinja na kumla nyama ni tukio la kusikitisha, Binadamu tunajua kwamba haliwi lakini huyu Mama anatuambia hivyo, tutamchukulia hatua kali"-Andrea Tsere, DC Ludewa.
#MillardAyoUPDATES