Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mourinho alikuwa akihusishwa na kibarua hicho cha kwenda kuinoa Arsenal, lakini sasa amekubali kuchukua mikoba ya kuinoa Spurs na sasa kuwafanya Mikel Arteta, Brendan Rodgers, Patrick Vieira, Max Allegri kupewa nafasi kubwa ya kwenda kuchukua mikoba ya klabu hiyo ya Emirates.
 
Na sasa Mourinho atakuwa kocha namba mbili anayelipwa mshahara mkubwa kwenye Ligi Kuu England, nyuma ya hasimu wake mkuu, Pep Guardiola anayelipwa Pauni 20 milioni kwa mwaka huko Manchester City. Pochettino ameondoka Spurs alikuwa akilipwa mshahara wa Pauni 7.5m milioni.
 
Kocha wa Chelsea, Frank Lampard mambo yake si haba, akivuna Pauni 5.5 milioni kwa mwaka, huku Brendan Rodgers huduma yake bora anayotoa huko Leicester City inawagharimu wakali hao wa King Power Pauni 5 milioni kwa mwaka na Eddie Howe analipwa Pauni 4 milioni kwa mwaka huko Bournemouth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…