Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sam Allardyce – timu 7

Sam Allardyce anayefahamika kama Big Sam ndiye kocha aliyefanya kazi kwenye timu nyingi za Ligi Kuu England kuliko yeyote, akizinoa timu saba. Kocha huyo ambaye amekuwa akiitwa kuokoa jahazi mambo yanapokuwa magumu, amefanya kazi kwenye timu za Bolton, Newcastle, Blackburn, West Ham, Sunderland, Crystal Palace na Everton.
 
Kocha Mark Hughes amekuwa na rekodi tamu pia kwenye Ligi Kuu England kwa kuwahi kuzinoa timu kibao. Hughes ambaye enzi zake alizokuwa mchezaji alitamba sana akiwa na Manchester United, lakini kwenye ukocha wake amezinoa timu sita tofauti kwenye Ligi Kuu England akipita kwenye timu za Blackburn Rovers, Manchester City, Fulham, QPR, Stoke City na Southampton.
 
Roy Hodgson – timu 5

Ukitaja orodha ya makocha waliozoweleka kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England basi Roy Hodgson jina lake huwezi kuliweka kando. Kocha huyo aliyewahi kuinoa pia timu ya taifa ya England, amepita kwenye timu mbalimbali akizinoa Blackburn, Fulham, Liverpool, West Brom na Crystal Palace na hivyo kufanya kuwa na timu tano alizowahi kuzinoa kwenye ligi hiyo.
 
Alan Pardew – timu 5

Kuna wakati Alan Pardew alikamatia vichwa vya habari huko England baada ya kukata viungo mbele ya kocha Arsene Wenger. Lakini, uhodari wa kocha huyo umemfanya apate nafasi ya kufanya kazi kwenye klabu nyingi akipita kwenye timu tano za Charlton, West Ham, Newcastle, Crystal Palace na West Brom. Pardew ni mmoja wa makocha wenye rekodi nzuri kwenye hilo la kunoa timu nyingi.
 
Steve Bruce – timu 5

Kwa sasa kocha Steve Bruce anapiga mzigo huko kwenye kikosi cha Newcastle United alipokwenda kuchukua mikoba ya Rafa Benitez. Hata hivyo, Bruce amekuwa kocha mzoefu kwenye Ligi Kuu England akizinoa timu tano tofauti kwenye ligi hiyo alipopita kwenye vikosi vya Birmingham, Wigan, Sunderland, Hull na Newcastle. Steve Bruce ana historia yake kwenye Ligi Kuu England na hivyo kuwa mmoja wa makocha wakongwe na wenye uzoefu mkubwa wa ligi hiyo.
 
Harry Redknapp - timu 5

Harry Redknapp kwa sasa ametulia zake, lakini ni mmoja wa makocha walioandika rekodi tamu kwenye Ligi Kuu England akipita kwenye timu nyingi ndani ya ligi hiyo. Bosi huyo matata kabisa aliyewahi kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Tottenham, amezinoa timu nne tofauti kwenye Ligi Kuu England ikiwamo West Ham, Portsmouth, Southampton, Spurs na QPR.
 
David Moyes – timu 4

Kocha David Moyes amepata umaarufu mkubwa zaidi baada ya kupata kazi ya kuinoa Manchester United. Miezi yake 10 aliyodumu na timu hiyo kabla ya kufutwa kazi ilimfanya kuwa maarufu zaidi. Hata hivyo, timu hiyo haikuwa ya kwanza kwa Moyes kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England akipita kwenye timu nne tofauti ndani ya ligi hiyo akianzia Everton, kisha Man United halafu Sunderland na kumalizia huko West Ham, ambako pia amefunguliwa mlango wa kutokea na kazi kupewa mwingine.
 
Neil Warnock – timu 4

Si jina geni masikioni mwa watu hasa kwa wale wanaoifuatilia Ligi Kuu England kwa undani zaidi. Neil Warnock ni mmoja wa makocha maarufu kabisa kwenye ligi hiyo akiwahi kufanya kazi kwenye timu nne tofauti wakati alipopita katika vikosi vya Sheffield United, QPR, Crystal Palace na Cardiff City. Kazi yake nzuri ndicho kitu kilichokuwa kikimfanya apate kazi kwenye timu nyingi licha ya kwamba timu alizopita ni zile za viwango vya kawaida.
 
Hata hivyo, kocha huyo ana umaarufu wake kutokana na sehemu alizokwenda kufanya kazi akiweka rekodi ya kuwa mmoja wa makocha waliofanya kazi kwenye zaidi ya timu tatu kwenye Ligi Kuu England, akiwahi kuzinoa Tottenham, Newcastle, Norwich na Brighton.
 
Graeme Souness – timu 4

Mashabiki wa Liverpool watakuwa na kumbukumbu nzuri ya kuhusu kocha Souness kutokana na kuwahi kupiga mzigo katika kikosi hicho cha wababe wenye maskani yake Anfield. Lakini, rekodi zake kwenye Ligi Kuu England, Sounnes zinazomeka kwamba alipita kwenye timu nnne tofauti akiwahi kuzinoa pia Southampton, Blackburn na Newcastle United, hivyo anakuwa kwenye ile orodha ya makocha wenye uzoefu wa kutosha wa kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England.
 
Rafa Benitez – timu 3

Mhispaniola, Rafa Benitez mara yake ya kwanza kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England ilikuwa huko Anfield alikotua kuinoa Liverpool.

Baada ya hapo aliondoka, kisha Chelsea walimchukua akapige mzigo kwao kabla ya kwenda kuinoa Newcastle United hivi karibuni, ambako pia aliondoka na kwenda kutafuta ulaji kwingineko.

Lakini, Benitez anakuwa mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa kwenye Ligi Kuu England kwa kufanya kazi katika zaidi ya timu moja, akipiga mzigo kwenye timu tatu tofauti ndani ya ligi hiyo.
 
Claudio Ranieri – timu 3

Mtaliano, Claudio Ranieri aliwaacha watu vinywa wazi wakati alipoisaidia Leicester City kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England kutokana katika mazingira ya aina yake.

Kocha huyo alikuwa na uzoefu wa Ligi Kuu England, kwa sababu kabla ya kibarua hicho cha King Power aliwahi kuinoa pia Chelsea huko nyuma kwenye ligi hiyo hiyo. Hivi karibuni, Ranieri alikuwa kwenye kikosi cha Fulham na kuwa timu yake ya tatu kuinoa kwenye Ligi Kuu England akijitengenea umaarufu mkubwa kwenye ligi hiyo.
 
Brendan Rodgers – timu 3

Rodgers kwa sasa anawakimbiza wapinzani wake kwenye Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Leicester City. Ubora wa kikosi hicho unamfanya ahusishwe na timu nyingi sana ikiwamo Arsenal na Manchester United. Lakini, kwenye ligi, kocha huyo amekuwa na uzoefu mkubwa akizitoa timu tatu tofauti kwenye Ligi Kuu England alipoanza na kikosi cha Swansea City kabla ya kupata dili huko Liverpool, akaondoka na sasa anatamba na Leicester City yenye maskani yake King Power.
 
Jose Mourinho – timu 3

Mreno, Mourinho amerudi kuwashika kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni mara yake ya tatu. Kwanza kocha huyo aliinoa Chelsea kwa awamu mbili tofauti kabla ya kupata kazi huko Old Trafford kuinoa Manchester United. Baada ya kufutwa kazi huko Old Trafford, Desemba mwaka jana, kocha huyo alisugua sana kijiweni kabla ya jana Jumatano kutajwa kuwa kocha mpya wa Tottenham Hotspur timu yake ya tatu kwenye Ligi Kuu England.
 
Makocha wengine

Kwenye orodha ya makocha walionoa timu zinazoanzia tatu kwenye Ligi Kuu England inawahusu pia George Graham (Arsenal, Leeds, Tottenham), Kenny Dalglish (Blackburn, Newcastle, Liverpool), Paul Jewell (Bradford, Wigan, Derby), Avram Grant (Chelsea, Portsmouth, West Ham), Glenn Hoddle (Chelsea, Southampton, Tottenham), Iain Dowie (Crystal Palace, Charlton, Hull), Martin O’Neill (Leicester, Aston Villa, Sunderland), Peter Reid (Man City, Sunderland, Leeds), Paul Lambert (Norwich, Aston Villa, Stoke), Gary Megson (Norwich, West Brom, Bolton), Joe Royle (Oldham, Everton, Man City), Dave Bassett (Sheff United, Nott’m Forest, Leicester), Tony Pulis (Stoke, Crystal Palace, West Brom) na Marco Silva (Hull, Watford, Everton)
 
Back
Top Bottom