Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ilivyokuwa Kiswahili ni lugha yangu ya kuzaliwa, basi ninaiandika kama ninavyoisema. Si shughuliki na "kua au kuwa, aliniambia au aliniambiya, ameuawa au ameuwawa kenda au kaenda, amekwenda au ameenda". Hayo kwa wataalamu wa lugha ni mambo muhimu lakini kwa mimi nakutakeni msamaha juu ya hayo. Muhimu ya kuyaangaliya na kuyazingatiya ni yale nikusudiayo kuyaeleza, kwani hayo ndio muhimu na ndio ya kweli tupu isiyokuwa na dosari hata chembe.
 
La mwanzo nitakalo kuombeni mlifahamu uzuri ni ile hakika kuwa hayo yaliyofanyika katika visiwa vyetu taarikh 12 Januari 1964, hayakuwa "MAPINDUZI" wala hayafai hata kidogo kuitwa 'mapinduzi' kwa maana asili ya neno. Bali kwa maana zote yalikuwa khasa ni "MAVAMIZI", yaani kwa Kiingereza "INVASION". Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwe na wananchi wenyewe kwa maslaha ya nchi na wananchi wake.
 
UTUKUFU NA NEEMA YA ZANZIBAR
Mwenyezi Mungu amevipa visiwa hivi viwili yaani Unguja na Pemba bahati ya utukufu kwa kila jambo lake. Hayo yaliendelea tokea karne na karne mpaka pale ulipotendwa ufisadi wa taarikh 12 Januari 1964, ndipo neema na utukufu wa Zanzibar ulipoanza kutoweka. Hapo tena, badala ya zumari kuwa likipulizwa Zanzibar, watu wa maziwani (Bara) walikuwa wakihemkwa, ikawa linapulizwa Bara, tuliopo visiwani tunahemkwa!
 
ZANZIBAR NA UBAGUZI KABLA YA MAVAMIZI
Nathubutu kusema bila ya wasiwasi wowote kuwa Zanzibar hakukuwepo ubaguzi wa namna yoyote kwa maana khasa na ya wazi ya neno UBAGUZI. Kwanza Wazanzibari ni watu waliochanganya sana damu hata sio rahisi kuweza kumtambua mtu kuwa ni mwenye kutokana na asili ya kabila fulani kwa kuangalia rangi yake au pua yake au masikio yake au kimo chake au kwa jina lake.
 
Jee, watu hao watabaguana namna gani? Malipo ya wafanyakazi serikalini yalikuwa hayakupangwa kiukabila. Wala serikali haikuwa na sehemu maalumu katika maskuli wala katika mahospitali kuwa zimetengwa kwa ajili ya watu wa makabila fulani. 6 Katika nchi za jirani zetu, Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwepo na ubaguzi uliyokuwa ukiongozwa na serikali za nchi hizo. Malipo ya mishahara ya wafanyakazi yalikuwa yakilipwa kutokana na makabila yao wala si kutokana na ujuzi wao wa kazi.
 
Kulikuwepo "African Scale, Asian Scale na European Scale". Madaktari, Mainjinia, Waalimu na wowote nawawe wana elimu na ujuzi na maarifa ya namna moja, yaani wote sawa sawa kwa elimu na ujuzi wa kazi zao, lakini mishahara yao ilikuwa tafauti kutokana na makabila yao.
 
Vyoo vya njiani (Public Toilets) na sehemu za kungojelea usafiri wa reli navyo vile vile vilikuwa vikitumika kwa ubaguzi wa kikabila. Waafrika waliekewa vyoo vyao na sehemu zao za kungojelea usafiri. Wazungu walikuwa na sehemu zao na Waasia walikuwa na sehemu zao, wote mbali mbali.
 
Lilikuwa ni kosa na kuvunja sheria ikiwa imetokea kwa yoyote kuingia katika sehemu isiyo kuwa amekhusika nayo. Khasa Muafrika awe ameingia au amekaa katika sehemu za Waasia au za Wazungu. Katika Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwa na Kodi ya Kichwa.
 
Kodi hiyo ilikuwa ikilipwa na kila mtu aliyekwishafika balegh katika umri wake. Nayo pia ikitekelezwa kwa njia za ubaguzi wa kikabila. Waasia na Wazungu, wao hata ikiwa wamechelewa kulipa kodi zao, basi walikuwa hawakamatwi majiani wala hawaendewi majumbani mwao kukamatwa
 
Lakini, Waafrika walikuwa wakisakwa majiani na wakiendewa majumbani mwao mnamo pinga pinga za usiku. Na wakikamatwa, basi walikuwa wakifungwa kamba za viunoni au hufungwa ncha ya shati la huyu na la huyu kisha walikuwa wakiongozwa mmoja nyuma ya mmoja na huku wakipigwa mateke na kusukumwa mpaka wakifikishwa Bomani.
 
Huko ikiwa hawatokuwa na cha kulipa basi walikuwa wakihukumiwa na kufungwa. Kutokana na hali kama hizo, ndipo wengi kati ya wananchi wa nchi hizo, khasa kutoka Tanganyika walikimbia kutoka makwao na kuhamia Zanzibar kwa sababu ya kufuata hali njema za kimaisha. Zanzibar hakukuwepo kodi za kichwa wala ubaguzi wa vyooni wala malipo ya mishahara wala wa namna yo yote. Ilikuwa njema atakae naaje.
 
UBAGUZI UMEANZISHWA ZANZIBAR WAKATI WA SERIKALI YENYE KUJIITA YA "MAPINDUZI"
Mara tu baada ya kufika hiyo serikali ya 'mavamizi' katika Zanzibar ubaguzi wa ukabila ulianzishwa. Kila "mrangi rangi" kama walivyokuwa wakiwaita wenyewe, yaani wenye asili za Kiarabu, za Kihindi na za Kingazija walianza kutolewa makazini bila ya kupewa hata haki zao za ufanyaji wa kazi.
 
Mashamba, majumba na hata mabiashara yao yalichukuliwa kwa nguvu na kupewa wageni ikiwa ni tunzo la ukatili na maovu waliyowafanyia wananchi katika nchi yao. Serikali ya 'mavamizi' ya Zanzibar ilitangaza rasmi kupitia vyombo vya khabari vya serikali kukhusu ubaguzi katika Taalimu. Waafrika, wakipasi au wasipasi bali idadi yao ya kuingia katika "Form One" ya "secondary school" ilikuwa ni 77 katika mia (77%), Waarabu 16 katika asili mia (16%), Wahindi 6 katika mia (6%), na Wangazija MMOJA katika mia! (1%).
 
Si hayo tu, bali serikali ya 'mavamizi' imetumia fedha za umma kwa ajili ya kujijengea hospitali yao wao tu Wanachama wa Baraza la Mapinduzi na familia zao na wameita, "Mapinduzi Wing". Vitanda, mabetishiti, foronya za mito, vyombo vya kulia kama sahani, vikombe, visu na nyuma (forks) vyote viliagiziwa kutoka Ulaya
 
Ilikuwa ikitokea Mheshimiwa kulazwa huko, basi na mkewe alikuwa akihamia huko huko na kulala kitanda kimoja kama kwamba wamo katika siku za fungati! Haya yakitendeka wakati wananchi wanyonge hawana hata dawa mahospitalini! Huo ulikuwa ndio usawa, sio ubaguzi!
 
ELIMU NA MATIBABU BURE!
Tunaambiwa na serikali yenye kujiita ya 'mapinduzi' kuwa elimu na matibabu yameanza kuwa bure kwa wananchi baada ya kupatikana kwa Serikali ya 'mapinduzi'! Huu ni uwongo uliokuwa hauna hata kifuniko.
Toka lini elimu na matibabu yalikuwa kwa malipo katika Zanzibar?
 
Tangu kuanzishwa kwa skuli ya serikali na Sayyid Ali bin Hamoud na toka kuanzishwa kwa matibabu katika mahospitali, kamwe hayajapata kuwa ya malipo. Toka kwa kuangaliwa na madaktari mpaka kwa madawa, chakula, na mpaka kulala kwa kutibiwa katika mahospitali kulikuwa bure.
 
TAALIMU Wananchi na wageni, kuanzia chumba cha kwanza yaani (standard one) mpaka kufikia chumba cha nane (standard eight), masomo yalikuwa bure kwa wote. Sio hivyo tu, kila mwanafunzi alikuwa na deski lake peke yake la kukalia na kila mwanafunzi alikuwa akipewa madaftari ya kuandikia bure, vitabu vya 7 kusomea bure, kalamu za kuandikia bure, vidawa vya wino na wino wake bure hata blotting papers (la kukaushia wino) pia wakipewa bure.

Na kila Ijumaa wanafunzi walikuwa wakipewa sabuni za kufulia bure. Skuli za mashamba, wanafunzi walikuwa wakipewa kifungua kinywa kunde na uji kabla ya kuingia katika vyumba vya masomo, bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…