Kwa ilivyokuwa Sheikh Othman aliahidiwa malipo fulani fulani kama vile kulipiwa deni la nyumba yake ya "Kijipu House" iliyokuwepo Gongoni, Zanzibar, na mengineyo yaliyokhusika na mambo ya kisiasa, aliukubali utumwa huo. Na kwa kuwepo makhusiano ya kuowana baina yake na Sheikh Mohammed Shamte, yaani Sheikh Mohammed Shamte alimuowa binti wa Sheikh Issa Shariff (mtoto wa kaka yake Sheikh Othman Shariff),
na vilevile mmoja katika hao washindi watatu wa ZPPP, alikuwa ni kaka yake yeye Othman, yaani, Sheikh Ali Shariff, basi Sheikh Othaman aliona itamuwiya rakhisi kufuzu utumwa huo. Othman aliingia mbioni kwa "Full speed".
Baada ya kuona jitihada zake zote alizozifanya za kumtaka Sheikh Mohammed Shamte ayakubali matakwa yake zimefeli, alianza kumtishia kaka yake Sheikh Ali Shariff kwa kumwambia kuwa, "Ikiwa na wewe hukubali kufuata shauri yangu, basi hutoniona tena baada ya leo. Afadhali nijiuwe kuliko kuona umeungana na Hizbu".