Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umma wote uliyokuwepo hapo, uliteremka uwanjani na kutujia katika sehemu tulizokuwa tumewekwa
na walipotufikilia, walitukumbatia kwa furaha kubwa na huku walikuwa wakitupa stahili salama.
Kufumba na kufumbua tulijiona tumeshatoka nje ya uwanja na hapo kila mmoja alichukuliwa na ndugu
pamoja na masahibu na wananchi wenzetu na tulitiwa katika mamotokari na kupelekwa majumbani
mwetu. Nilipo fika nyumbani nilipokelewa na ahli zangu kwa furaha na kwa hoihoi pamoja na kuvunjiwa
nazi ikiwa ni "DafaalBalaa".
 
KUULIWA WANANCHI MSIKITINI
Mnamo taarikhi 9 Septemba, 1964 katika kiasi cha saa tatu za usiku, mmoja katika wakuu wa Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar, Mohammed Abdalla Kaujore, baada ya kupiga bangi zake na kunywa ulevi wake aliwaingilia wananchi waliyokuwa wakifanya ibada zao ndani ya Msikiti wa Ithinaashiri wa Kiponda na kuwauwa kwa kuwapiga marisasi bure bilashi. Watu watano waliuwawa siku hiyo. Mmoja kati ya hao alikuwa mtoto wa miaka minane akiitwa, Abbas Kassim. Wengine walikuwa, Seyyid AbdulMuttalib Hashim, Seyyid Ali Asghar, Haj AbdulHusain Tejani na Babu Haji.
 
Edington Kisasi akiwa miongoni wa wakuu wa hiyo Serikali ya Mavamizi na ndiye wakati huo aliyekuwa mkuu wa Polisi, alitangaza katika Radio ya Zanzibar, "Serikali inasikitishwa sana kwa kitendo kilicho fanyika katika Msikiti wa Ithinashiri, Kiponda. Na Serikali inafanya uchunguzi juu ya tokeo hilo na mara tu baada ya kupatikana matokeo ya uchunguzi huo, Serikali itachukuwa khatua za kutosha juu ya ukhalifu uliyo tendeka". Mpaka naziandika khabari hizi ndani ya hiki kijitabu, imeshapita miaka 30 tokea kutokea tokeo hilo, na hata hilo uwaji lenyewe nalo limesha kufilia mbali, na bado Serikali ya Mavamizi haijaweza kutoa natija ya hakika juu ya huo uchunguzi waliyokuwa wameusema kuwa waufanye! Katili hilo liliachiliwa likitembea kwa marefu na mapana kama kwamba halikufanya lolote,bali lilibaki katika cheo chake vilevile. (Mwizi mgema, askari mgema, na hakimu mgema. Jee mwenye mnazi atapata haki hapo?)
 
KUULIWA KWA WANANCHI WENGINE
Baada ya kumalizika mavamizi hayo Jamuari, 1964 na yakatendwa yaliotendwa, tangu kwa kuuliwa na kwa kudhalilishwa kwa kila aina, haikutosha bali daima wananchi wakitishwa na kukamatwa kamatwa ovyo. Katika mwaka 1964, Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar kama kawaida yake iliwavamia na kuwakamata baadhi ya wananchi. Wananchi hao wengine walikamatwa kutoka majumbani mwao, wengine kutoka makazini mwao na wengine mabarabarani. Baada ya kuwakamata kwanza waliwapeleka kwenye kituo cha Jeshi cha Mtoni na baadae waliwaondoa, wengine walipelekwa kwenye Makao Makuu ya Magereza, Kiinua Miguu na wengine walipelekwa kwenye kituo cha Kijeshi "Army House", kilichokuweko huko Migombani.
 
Miongoni mwa waliokamatwa wakati huo walikuwa Mabwana hawa: (akiwemo bibi mmoja) Muhammed Salim (Jinja) Amour Zahor Said Dahoma (Kombanyongo) Mohammed Hamoud Barwani Nasser Mansour Musa Ahmed (Lashoka) Sultan Binbrek Ali Mohammed Barwani Bibi wa Unguja (Mke wa Bwana AbdulRahman Haider[ Maalesh]) Mohammed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed, wao ndiwo walioondolewa kutoka Makao Makuu ya Magereza na kupelekwa "Army House". Tokea siku hiyo waliyoondoshwa kutoka Makao Makuu ya Magereza hadi hii leo hawa jaonekana tena. Kutokana na khabari zenye kuaminika na hao wenziwao waliyokuwa pamoja wakati huo zinasema kuwa wote hao 53 yaani Mohammmed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed, wameuliwa siku moja katika sehemu ya Kama, Unguja kwa kupigwa risasi.
 
Kabla ya kuuliwa, kwanza walitakiwa wao pamoja na hao wenziwao, wachimbe shimo kubwa liwe ndio kaburi lao, yaani wajichimbie wenyewe kaburi lao. Baada ya kumaliza kulichimba, aliitwa kwanza, Sheikh Mohammed Salim Jinja na alitakiwa avuwe nguo zote hata chupi, na alizivua. Baada ya kuzivua, alipewa kalamu na karatasi aandike wasia ikiwa anapenda. Sheikh Mohammed alikataa kuandika. Aliambiwa afungue kinywa na baada ya kufungua, alitiwa bastola kinywani na alifyatuliwa risasi humo humo kinywani. Hapo hapo alikufa na alisukumwa ndani ya hilo shimo.
 
Hahahahaah [emoji23][emoji23]
Ni katika harakati za ushabiki.
Nashabikia ushindi ipasavyo[emoji1787][emoji1787]

Naisubiri siku ya kufungwa,SYB ataniua kwa kunizomea[emoji23]
Unashangilia hadi majirani tunatamani kushangilia na wewe[emoji51][emoji23][emoji23]!


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yani kama namuona huko anakuandalia mabango yako.!!
 
Baada yake, wapili alikuwa Sheikh Amour Zahor. Yeye vilevile alitakiwa avue nguo zote, alizivua, ila yeye alikataa kuvua chupi. Yeye aliwekewa bastola juu ya kifua upande wa mkono wa kushoto na ilifyatuliwa risasi. Sheikh Amour yeye alikaiwia kidogo kufa, na alitumbukizwa shimoni akiwa bado anatweta. Mwengine, aliyefuatia kuuliwa alikuwa, Sheikh Mohammed Hamoud na baada yake alifuatia, Sheikh Said Dahoma Kombanyongo na wa mwisho alikuwa Seyyid Hamza Mohammed. Wenziwao waliyokuwa pamoja nao katika siku hiyo, walikuwa, Mabwana Nasser Mansour, Musa Ahmed (Lashoka), Ali Awadh, Awadh Salim, Idi Juma, Said Ali Hamoud AlHarthy, AbdulRahman Haider (Maalesh), Sultan Binbrek na Bibi wa Unguja. Walitakiwa wawafukie wenziwao ndani ya hilo shimo walimotumbukizwa likiwa ndio kaburi lao.
 
Huyu msukuma siku nikifungwa alisema atanifungia safari Hadi tukuyu.
Akija kunizomea na zile hasira zangu za kufungwa nambangua na parachichi kisogoni[emoji23][emoji23][emoji23]
Unashangilia hadi majirani tunatamani kushangilia na wewe[emoji51][emoji23][emoji23]!


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yani kama namuona huko anakuandalia mabango yako.!!
Nashabikia kwa sababu Jana sikushabikia vizuri..nilikuwa na wenge la usingizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…