Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchakato wa kocha mpya wa sasa, kwa sasa ulipofikia ni kuwafanyia mahojiano kocha mmoja baada ya mwingine, huku ikidaiwa kwenye orodha hiyo yupo kocha wa zamani wa Valencia, Marcelino na kocha msaidizi wa Pep Guardiola huko Manchester City, Mikel Arteta.
 
Lakini, mambo yamenoga zaidi baada ya Napoli kumfuta kazi kocha wake Carlo Ancelotti na moja jambo hilo limewafanya Arsenal kufikiria kumpa kazi Mtaliano huyo, wakijaribu kuufanyia kazi ushauri wa kocha wao wa zamani, Arsene Wenger aliposema Arsenal sasa inahitaji kocha mwenye uzoefu.
 
Jina la Thomas Tuchel wa Paris Saint-Germain naye ametajwa kama wababe hao wa Ufaransa wataamua kuachana naye, lakini mpango wote upo chini ya mkuu wa soka Raul Sanllehi na mkurugenzi wa ufundi Edu sambamba na mkurugenzi Vinai Venkatesham pamoja na mtaalamu wa mikataba Huss Fahmy kuamua ni kocha gani anayestahili kutua Emirates kwenda kuchukua mikoba ya Unai Emery.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…