Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jambo hilo liliibua malumbano makubwa kwenye timu na Yaya alisugua sana benchi, shukrani kwa wachezaji wenginne wa sehemu ya kiungo kupata majeruhi na hapo Guardiola hakuna na ujanja zaidi ya kuanza kumtumia mchezaji huyo. Hata hivyo, Yaya hakuwa tena yule aliyekuwa akiwapa raha mashabiki wake na kumfanya aondoke kwenye timu hiyo akiwa na huzuni tofauti na ambavyo angeondoka kabla ya Guardiola kutua kwenye timu hiyo.
 
Robin Van Persie v David Moyes (Man United)

Sir Alex Ferguson alimsajili straika Robin Van Persie kutoka Arsenal mwaka 2013 na Mdachi huyo baada ya kutua Old Trafford tu alifunga mabao 26 katika mechi 38 alizocheza kwenye Ligi Kuu England na kuisaidia Manchester United kubeba taji lake la 20 la ligi, ambalo ni la mwisho pia kubeba, tangu wakati huo hawajabeba tena.
 
Lakini, furaha ya Van Persie kutamba kwenye timu hiyo ilidumu kwa msimu mmoja tu, kwani Ferguson alipostaafu na David Moyes kuja kuchukua mikoba basi kila kitu kilibadilika. Moyes alikuwa akimtumia hovyo mshambuliaji huyo hakumwezea kitu ambacho kilimfanya Van Persie kuanza kucheza chini ya kiwango na kuamua kuondoka zake kwenda Fenerbahce. Mashabiki wa Man United waliamini katika huduma ya Van Persie, lakini kwa kiwango chake alichokuwa akicheza chini ya Moyes, kiliwashangaza na mchezaji mwenyewe aliamua kuondoka kabla ya mambo hayajatibuka zaidi.
 
Maisha ya straika Romelu Lukaku yalikuwa matamu kwelikweli huko Manchester United alipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho. Panga pangua Mbelgiji huyo alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Mourinho akiwa straika chaguo la kwanza la Mreno huyo huko Old Trafford. Lakini, baada ya ujio wa Ole Gunnar Solskjaer tu kwenye kikosi hicho kila kitu kilitibuka, Lukaku akaanza kuchezeshwa pembeni na sio mshambuliaji wa kati tena. Mara akaanza kuonja benchi mechi moja moja kabla ya fowadi huyo kuamua kuondoka kwenye timu hiyo akitimkia zake Inter Milan kabla ya mambo hayajatibuka sana chini ya kocha mpya.
 
Christian Benteke v Jurgen Klopp (Liverpool)

Straika mwingine wa Kibelgiji, Christian Benteke alikuwa moto huko Aston Vila na kuwafanya Liverpool kutoa pesa kunasa saini yake. Maisha yake ya Anfield yalikuwa safi wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya Kupatikana kwa huduma ya mshambuliaji huyo kuliwapa Liverpool matumaini ya kufanya vizuri zaidi. Lakini, jambo hilo lilitokea wakati Liverpool ilipokuwa chini ya kocha Brendan Rogers.
 
Hata hivyo, Rodgers alipoonyeshwa mlango wa kutokea na Jurgen Klopp kuja kuchukua mikoba yake, hiyo ilikuwa habari mbaya kwa straika Benteke, ambapo maisha yake hayakuwa mazuri kabisa chini ya kocha mpya. Taratibu akaondolewa kwenye kikosi cha Klopp akachukua wachezaji wake akiwamo Mohamed Salah na Benteke akasukumiziwa Crystal Palace.
 
Rafael da Silva v Louis van Gaal (Man United)

Mashabiki wa Manchester United hawakuelewa kabisa kwanini Louis Van Gaal aliamua kumpiga bei beki pacha wa Kibrazili, Rafael da Silva. Van Gaal alimpiga bei staa huyo kwenda Olympique Lyon na kuwafanya mashabiki wa Man United kushangaa. Lakini, ukweli ni kwamba ni wakati mbaya tu aliokutana nao Rafael chini ya kocha mpya.
 
Kocha Sir Alex Ferguson alikuwa kipenzi kikubwa cha beki huyo mambo yalikuwa hivyo pia chini ya David Moyes, lakini kila kitu kilikuja kuwa tofauti baada ya ujio wa Van Gaal kwenye timu. Rafael alionekana hafai na hivyo kuondoshwa kwenye timu.
 
Joe Hart v Pep Guardiola (Man City)

Timu kibao zilikuwa zikitamani kuwa na huduma ya kipa Joe Hart kwenye vikosi vyao, lakini utashangaa kocha Pep Guardiola alipotua tu Manchester City alimwona kipa huyo hafai. Kwanza akaanza kwa kumtoa kwa mkopo kipa huyo na taratibu akamwondoa kabisa huku akiwaleta kina Claudio Bravo, ambao pia walishindwa kufanya vizuri huko Etihad.
 
Guardiola alifanya usajili wa makipa mfululizo baada ya kumwondoa Joe Hart kwa kumpeleka kwa mkopo Torino na kumnasa Bravo mambo yalikuwa magumu hadi hapo alipofanya usajili wa Ederson, ambaye ndiye chaguo lake la kwanza kwa sasa. Lakini, ukweli wa kuhusu Joe Hart kitendo cha kushindwa kuaminika na Guardiola kilimsababishia matatizo makubwa kisaikolojia na hakuwa fiti tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…